UFISADI HAUKUBALIKI NDANI YA NCHI HII
Nimeamua kuzungumzia swala la ufisadi ambalo kila mtanzania limekuwa kilio kwake. Neno ufisadi limekuwa kama msiba ndani ya nchi yetu na hata dunia nzima, Serikali pamoja na wananchi wamejitahidi kupambana na na ufisadi lakini angalau kidogo kinga imeweza kupatikana katika serikali ya awamu ya nne, japokuwa dawa ya ugonjwa huu hatari kwa jina maarufu ufisadi haijapatikana. Tumeweza kuona majina mengi ya viongozi wa umma yakitajwa kwa ufisadi. Mimi kama Denis kila siku namuomba Mungu atutatulie hili janga ambalo linasababisha Watanzania wengi wanaishi katika maisha magumu yanayosababishwa na watu wachache wakijinufaisha kwa masilahi ya wachache. Tunaweza kusema hili janga ni la dunia nzima lakini wenzetu wan chi za Ulaya, Asia na America wamejitahidi kuweka sheria kali ambazo zitawabana hawa watu wanaodidimiza uchumi wa nchi. Tumeona serikali ya chini imeamua kuingiza sheria kali kwenye katiba yao kwa ajili ya kuwabana mafisadi. Ningeomba Serikali yangu ya Tanzania ikishirikiana na Wananchi walichukulie hili swala kama janga la kitaifa ambalo mimi nalifananisha na ugonjwa unaotisha wa Ebola, ambao unaua mapema sana. Naipenda sana nchi yangu Tanzania kisiwa chenye amani, rasilimali za kutosha lakini wananchi wanateseka na gonjwa la ufisadi, naliomba bunge letu tukufu liweze kutunga sheria ambayo itawafanya hawa wajanja wachache wasiweze kupata mwanya wa kuendeleza mchezo huu mchafu, ambao bila uoga na hata kumuogopa Mungu wanaamua kuwasliti wanaowatumikia na kuingizia Serikali hasara na kusababisha nchi kuwa masikini kwa masilahi yao binafsi, nipo tayari kushirikiana na serikali pamoja na taasisi mbalimbali kupambana na janga hili hatari la ufisadi, kwani swala hili si la serikali tu bali letu sis wote watanzania wenye uchungu na uzalendo wa nchi yetu iliyojaliwa kila aina ya baraka, zipo mbuga za wanyama zenye kila aina ya wanyama, madini ya kila aina na kujivunia kuwa na Tanzanite inayopatikana Tanzania peke yake, mlima mrefu kuliko yote Africa ambao unapatikana Tanzania, mito milima na maziwa na bahari ya kuvutia. Naweza kusema mimi binafsi nashuru sana serikali ya awamu ya nne ikiongozwa na Rais wetu mpendwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuonyesha uzalendo wake kutangaza vita dhidi ya ufisadi na hatimaye kuwafungua macho baadhi ya watanzania ambao hawakuwa wanajua kama rasilimali zao zinachukuliwa na wachache. Amejaribu kuweka uhuru wa maoni, midahalo ya hapa na pale, demokrasia makini pamoja na utawala wa sheria. Hata hivyo tusilale tupambane mpaka ushindi upatikane na kuipata dawa ya janga hili hatari., nimejaribu kuchunguza na kuona kuwa nchi changa hasa za bara la Afrika ndizo zinazoongoza janga la ufisadi. Pia ningeomba umoja wa Africa pamoja na wananchi wote wa Afrika walichukulie kama janga linalotisha duniani, tukiwa na ushirikiano baina ya Wananchi na Serikali pamoja na taasisi mbalimbali tutaibuka na ushindi na mwisho tutakuwa na Tanzania yenye maendeleo, maisha bora, utawala bora, kukomaa kwa uchumi, pamoja na kufikia malengo yetu yenye mafanikio mazuri.
Mwisho mimi kama Denis, naiomba serikali ijaribu kuhamasisha viongozi wake wa umma pamoja na taasisi zote za ndani na nje haijalishi taasisi za kiserikali au binafsi kwa kushirikiana na wananchi, kuuchukia ufisadi popote pale iwe kanisani, misikitini, maofisini, kwenye vyombo vya habari, mashuleni, hotelini, taasisi mbalimbali, vyombo vya usafiri, vyombo vya usalama na popote pale shughuli za serikali zinapofanyika tuwe na kauli moja inayosema “Ufisadi basi”, ‘Ufisadi haukubaliki’ ‘Ufisadi haukubaliki’ ‘Ufisadi haukubaliki’
Denis Bahati Hendry.
Nipigie- 0712 550 508
-0765 002 472
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
Ni mimi mpenda maendeleoDenis Bahati Hendry.
Nipigie- 0712 550 508
-0765 002 472
No comments:
Post a Comment