Header Ads

Maendeleo ya miundombinu: Nguzo ya uwezeshaji katika kufikia uchumi imara

Mkurungezi Mtendaji wa Buzwagi Gold Mine Bw; Stewart Hamilton akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa Uwanja wa ndege wa Buzwagi na pembeni yake ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ambao kwa kwa kiasi kikubwa ACACIA wamewekeza katika kuboresha uwanja huo.
Wananchi wa Kahama wakishuhudia uzinduzi wa safari za ndege za shirika la Precision Air katika uwanja wa ndege wa Buzwagi.


Mazingira mazuri ya kukuza uchumi yanahitaji miundombinu bora inayowezesha uchukuzi huku ikiboresha uzalishaji na ufanisi. Hivi karibuni, wakazi wa Kahama na Shinyanga watafurahia safari za ndege kati ya Kahama na Dar es Salam. Haya ni matokeo ya ushirikiano wa Acacia Mining ulioanza toka mwaka 2008, ilipoanza uzalishaji katika mgodi wake wa Buzwagi; huku wakiendelea kuwekeza katika kiwanja cha ndege cha Kahama, wakihakikisha kiwanja kinatunzwa na kufanya kazi. 
Ushirikiano wa karibu kati ya Mkuu wa Wilaya Mh. Fadhil Nkurlu na Mgodi umewezesha kuanzishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja. Safari za shirika la ndege la Precision zitapunguza adha ya usafiri ya wakazi wa Kahama na Shinyanga waliotakiwa kusafiri hadi Mwanza ili kupata usafiri wa ndege kuelekea Dar es Salaam.
 ‘Hii itasaidia sana kuongeza ufanisi katika muda na fedha zinazotumika katika usafiri,’ alisema mfanyabiashara Bw. Charles Thomas akiongeza kuwa safari ya barabara hadi Mwanza ingeweza kuchukuwa hadi masaa 6. Kufuatia mafanikio ya safari ya majaribio mwezi uliyopita, Meneja Mahusiano wa Kampuni wa shirika la ndege la Precision, Bw. Hillary Mremi alisifia hali ya kiwanja akisema, ‘njia ya ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Buzwagi ipo katika hali nzuri na matunzo yake ni mazuri; hii ni nzuri kwa usalama wa abiria na ndege zetu. 

Tunashukuru Acacia kwa kuwekeza katika kuboresha, kiwanja kidogo cha Buzwagi; hatua iliyoturuhusu kuanza safari kuelekea Kahama, zitakazo anza 5 September, 2017, tukiwa na safari tatu kwa wiki, na safari zikiongezeka zikitegemea mahitaji ya wasafiri. Hatua ya kutatua shida ya miundombinu ni moja itakayoleta matokeo chanya kwa biashara mkoani Shinyanga kwa kupunguza gharama za kuendesha biashara; huku ikiongeza faida.

Japokuwa Acacia imefanya uwekezaji wenye tija katika kuendeleza na kurekebisha kiwanja hiki kidogo cha ndege, ni muhimu kukumbuka kwamba kiwanja hiki ni mali ya Serekali chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Uwekezaji katika kiwanja hiki kidogo inaonyesha nia ya Acacia kuendelea kusaidia jamii na taasisi zinazozunguka migodi yake.

No comments:

Powered by Blogger.