DK. SALIM KUZINDUA KITUO CHA UTAFITI NA MAFUNZO YA UYOGA CHA CHUO KIKUU CHA KAIRUKI
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maadhimisho ya
17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert Kairuki yatakayofanyika kuanzia
Februari 4. Kushoto ni Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni.
Makamu
Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN), Dk. Muganyizi
Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert Kairuki
yatakayofanyika Februari 4. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo cha
Kumbukumbu ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni na Ofisa Habari wa chuo
hicho, Abraham Mwalugeni.
…………………………………
Katika
kuadhimisha miaka 17 ya kumbukuzi ya mwaasisi wa chuo kikuu cha
kumbukumbu ya Hubert kairuki kuanzia tarehe 4 hadi 6 Feb ambayo
itakuwa ni siku ya kilele.Mh Dr Salmin
Ahmed
Salim ambaye pia ndio mkuu wa chuo hicho atazindua jengo la utafiti
na mafunzo ya Uyoga lililopo huko Boko katika eneo la chuo hicho.
Sambamba
na uzinduzi huo pia shughuli nyingine katika kumbukizo hizo itakuwa
ni pamoja na muhadhara kuhusu Uyoga utakaotolewa na Profesa Keto
Mshigeni ambaye ndiye makamu mkuu wa chuo hicho na mwanasayansi
aliyebobea katika tafiti za uyoga.
Pia hospital ya Kairuki it ataendesha zoezi maalum la upimaji na matibabu ya macho
bila ya malipo kwa siku mbili mfululizo. Pia patakuwepo matembezi
ya hiara kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya saratani ya
kizazi.
Aidha
wanafunzi wa zamani wa chuo hicho waliopo Mwanza na mikoa ya kanda
ya ziwa wataadhimisha kumbukizo hizo kwa kufanya zoezi la kupima
afya bure kwa wakazi wa huko.
No comments:
Post a Comment