NAIBU KAMISHNA MKUU WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Uongozi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ukiwa katika kikao na Ujumbe wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) uliotembelea
Wizara hiyo. Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, John Mngodo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo
akizungumza na ujumbe wa Shrika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR) (haupo pichani) uliotembelea Wizara hiyo ambapo
masuala mbalimbali kuhusiana na wakimbizi yalijadiliwa. Tanzania ni
mojawapo ya nchi zinazohifadhi wakimbizi, hasa kutoka Ukanda wa Maziwa
Makuu.
Naibu
Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR), Bi. Kelly Clements akizungumza katika kikao na Uongozi wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (haupo pichani) wakati yeye na ujumbe
wake walipotembelea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Katikati ni
Mkurugenzi wa UNHCR, Kanda ya Afrika na kushoto ni Mtendaji Msaidizi wa
Naibu Kamishna Mkuu wa UNHCR, Bi. Geraldine Salducci.
Mkurugenzi
wa Idara ya Wakimbizi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison
Mseke akizungumza katika kikao cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na
ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)
wakati ujumbe huo ulipotembelea Wizara. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi).
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment