Header Ads

VIJANA CCM WAJITOKEZA KWA WINGI KUCHUKUA FOMU ZA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI.

Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Priscus Tarimo,akikabidhiwa fomu ya nafasi hiyo na katibu wa CCM manispaa ya Moshi,Loth Ole Nesele katika ofis za chama hicho za Wilaya ya Moshi mjini.
Mtia nia ya kugombea Ubunge jimbo la Moshi mjini,Priscus Tarimo,akitoa maelezo yake kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya Moshi mjini Donatha Mushi alipofika kwa ajili ya zoezi la uchukuaji wa fomu.
Priscus Tarimo akizungumza na na wanahabari( hawako pichani) muda mfupi baada ya kumaliza zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania kuteuliwa katika nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM jimbo la Moshi mjini.
Naibu kamanda wa Vijana wa CCM,manispaa ya Moshi ,Edmund Rutaraka akipokea fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kutoka kwa katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Moshi mjini,Donatha Mushi.

No comments:

Powered by Blogger.