Zantel yatoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania
Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans
Tegete akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa kisima kwa
ajili ya kituo chake kutoka kwa kampuni ya Zantel. Kushoto kwake ni Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel,
Pratap Ghose
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda
akizungumza wakati wa kukabidhi kisima kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Zantel, Pratap Ghose.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
akizindua kisima cha maji kilichojengwa na kampuni ya simu ya Zantel kwa ajili
ya kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
Kampuni ya simu ya Zantel leo imetoa msaada
wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na
lengo la kumaliza tatizo la maji na kuhakikisha
upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo
hicho.
Tatizo
la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na
Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.
Kisima
hicho kilichokabidhiwa leo kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa
matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na
maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.
Akizungumza
wakati wa makadhiano, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose
alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu
kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya
kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka
‘Kampuni
yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua
kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya
matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’ alisema Pratap.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Mheshilmiwa Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya
makabidhiano, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara
inayofaa kupongezwa.
‘Ustawi wa watoto na vijana ni jambo muhimu
katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia
kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito
kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.
Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilianzishwa
mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata
matunzo na elimu bora.
Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu
Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini
sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.
‘Awali tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo
upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua
tatizo hili’ alisema Tegete.
No comments:
Post a Comment