MGIMWA AWAKUNA WAZEE NYAMIHUU WAMCHANGIA TSH 100,000 YA FOMU YA UBUNGE

Mbunge
wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akishuka katika pikipiki (Boda Boda)
akitoka kukagua ujenzi wa zahanati kijiji cha Nyamihuu leo.
Mbunge
wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akikabidhi saruji mifuko 60 kwa
mwenyekiti wa kijiji cha Nyamihuu Bw Richard Mbembe kwa ajili ya ujenzi
wa zahanati ya kijiji kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake.
Na matukiodaimaBlog
WAZEE
wa kijiji cha Nyamihuu kata ya Nzihi wamempongeza mbunge wa jimbo la
Kalenga Godfrey Mgimwa kwa kumchangia Tsh 100,000 ya kuchukulia fomu
tena ya ubunge baada ya kuwatumikia vizuri kwa muda wa mwaka mmoja wa
ubunge wake .
Wakitoa
pongezi hizo leo wakati wa ziara ya mbunge huyo kumalizia ahadi Yake ya
Bati 60 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ,walisema kuwa
wamevutiwa na chapakazi wake alioonyesha katika kipindi chake kifupi cha
mwaka mmoja.
Akizungumza
kwa niaba ya wazee hao na wananchi wa Kijiji cha Nyamihuu Bi shekela
Mvela alisema wamelazimika kuchangishana kila mmoja kiasi cha Tsh
10,000 na kufikisha kiasi hicho cha Tsh 100,000 kama ahsante Yao kwa
mbunge huyo.
Hata
hivyo walisema imani kubwa ambayo wao wameionyesha kwa mbunge huyo ni
wazi ni imani ya wananchi wote wa jimbo hilo ambao wamepata kushuhudia
Kazi nzuri iliyofanya na mbunge huyo kijana kwa muda mfupi zaidi
ukilinganisha na wabunge waliotangulia ambao walikuwa wakiahidi pasipo
kutimiza
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Nzihi Steven Mhapa mbali ya kumpongeza
mbunge huyo kwa utekelezaji wa ahadi zake bado alisema CCM itaendelea
kushinda katika jimbo hilo kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani
uliofanyika.
Kwa
upande wake mbunge Mgimwa ambae alipokelewa kwa maandamano ya Boda Boda
katika kijiji hicho cha Nyamihuu alisema amefarijika zaidi kwa upendo
mkubwa ulioonyeshwa na wananchi hao wa Nyamihuu pia mchango wao wa fedha
ya kuchukulia fomu
Alisema
kuwa wapo ambao wanaeneza uvumi kuwa hatagombea tena ubunge jambo
ambalo si kweli isipo kuwa baada ya bunge kuvunjwa atachukua fomu tena
ya ubunge ili kupata kipindi chake cha miaka mitano ya kuwaletea
maendeleo wananchi hao wa jimbo la Kalenga .
mbunge
Mgimwa alitaja ahadi mbali mbali zilizokuwa zimebaki kata ya Nzihi na
kuzitekeleza leo kuwa katika kijiji cha kipera amekabidhi Tsh 500,000
kwa kikundi cha Umoja PTC, Kwaya ya mtakatifu Thomas Nzihi amekabidhi
Tsh milioni 1, kanisa la TAG nzihi Bati 44 ,kijiji cha Nyamihuu mifuko
60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji na Kidamali Tsh
milioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa ghala la kijiji.
Alisema dhamila Yake ni kutimiza ahadi zake zote ndani ya siku mbili hizi ili anapogombea tena ubunge asiwe na kiporo cha ahadi.
No comments:
Post a Comment