Header Ads

KAMPUNI YA MABATI YA AFRICAN ALLUMIUM (ALAF), IMEZINDUA MABATI AINA YA ROYAL VERSATILE

Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabati ya Alluminium Afrika (Alaf), Yahya Ngoza akizungumza na mmoja kati ya wateja waliotembelea banda hilo, wakati wa Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere barabara ya Kilwa.

 Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabati ya Alluminium Afrika (Alaf), Monica Reuben akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliofika katika banda la kampuni hiyo, wakati wa Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere barabara ya Kilwa.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. 
 Kampuni ya Mabati ya African Allumium (Alaf), imezindua mabati mapya aina ya Royal Versatile ambayo yana uwezo mkubwa wa kuhimili kutu na mazingira mengine ya hali ya hewa popote nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabati hayo, Meneja Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy alisema kuwa mabati hayo yamezinduliwa rasmi wakati wa maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, barabara ya Kilwa.
Alisema mabati hayo ambayo yana viwango vya kimataifa na yameanza kuuzwa pia nje ya nchi, yanamudu mazingira yote ikiwa ni pamoja na ukanda wa Pwani ambako hali ya hnewa yake ina kiwango kiklubwa cha chumvi.
“Maeneo mengine ni lazima ujenge na vigae na sio bati kutokana na kiwango kikubwa cha chumvi katika hewa” alisema na kuongeza kuwa hali hiyo husababisha mara nyingi kutu katika mabati hivyo kuyasababishia kuharibika katika kipindi kifupi.
Alisema utalaam na teknolojia iliyotumika katika utengenezaji wa mabati hayo unafanya  Tanzania kama Taifa kuwa na eneo la kujivunia katika sekta ya ujenzi tofauti na siku za nyuma.
“Tuna bidhaa ambayo inaweza kushindana kimataifa na pia kupanua wigo wa biashara katika nchi za Afrika Mashariki, Kat8i na Kusini” alisema Mmasy.
Kampuni hiyo ambayo asilimia kubwa ya hisa zakwe zinamilikiwa na serikali, imetoa punguzo maalum kwa wateja ambao watanunua mabati hayo wakati wa maonyesho hayo, lengo likiwa kuchangia pato la Taifa na kusaidia ujenzi wa nyumba bora nchini.

No comments:

Powered by Blogger.