MAFUNZO YA TAKWIMU KWA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA ARUSHA
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Takwimu nchini Dr Albina Chuwa akiongea na vyombo vya
habari jijini Arusha katika mafunzo ya siku tano kuhusu suala la
takwimu zinazohusu hali ya mazingira, ikiwemo uharibifu unaotokana na
uchafuzi wa maji, hewa chafu na kupotea kwa uoto wa asili ,Mafunzo hayo
yameudhuriwa na viongozi kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
(Habari Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkuu
wa kitengo cha takwimu katika Umoja wa Mataifa, Reena Shah amesema
idara yake ina mkakati maalum wa kusaidia nchi hizo katika ukusanyaji wa
takwimu za mazingira ambazo kwa sasa ni muhimu sana katika kuweka
ajenda na mipango ya maendeleo endelevu.
Mkurugenzi wa Takwimu Nchini Burundi Mohamed Feruz akizungumza na vyombo vya habari kuhusu takwimu katika nchi yake
Washiriki wakifwatilia mafunzo kwa ukaribu zaidi
Washiriki wa mafunzo ya Takwimu kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Meneja wa idara ya Takwimu Mkoani Arusha Margeret Mutaleba akizungumza katika mafunzo hayo jijini Arusha
Prof.Innocent Ngalinda akizungumza katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Takwimu nchini Dr Albina Chuwa amesema kuwa suala la
takwimu zinazohusu hali ya mazingira, ikiwemo uharibifu unaotokana na
uchafuzi wa maji, hewa chafu na kupotea kwa uoto wa asili bado ni ngeni
katika nchi zinazoendelea, hususan za bara la Afrika na kwamba kuna
umuhimu wa kutoa mafunzo maalum kwa wafanyakazi wa idara za takwimu
nchini.
Aliyasema
hayo jana wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa nchi za Jumuiya ya
Afrika mashariki jijini Arusha uliohudhuriwa na viongozi wa Takwimu wa
nchi hizi.
Bi.Chuwa
alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia hali ya tabia nchi na mazingira
huku akisisitiza kuwa Takwimu za mazingira zinahitaji watu wawe na uwezo
mkubwa yaani elimu pamoja na rasilimali fedha na vifaa huku akitoa rai
kwa Jumuiya ya Afrika mashariki kuangalia tasnia hiyo kwa kupewa
kipaumbele kama sekta zingine.
Naye
mkuu wa kitengo cha takwimu katika Umoja wa Mataifa, Reena Shah amesema
idara yake ina mkakati maalum wa kusaidia nchi hizo katika ukusanyaji
wa takwimu za mazingira ambazo kwa sasa ni muhimu sana katika kuweka
ajenda na mipango ya maendeleo endelevu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Takwimu nchini Burundi Mohamed Feruz alisema
kuwa katika nchi yake bado hawajaweza kuwa na vifaa vya kisasa vya
kuweka kumbukumbu
“Hatujapata mafunzo ya namna ya kufanya hizi takwimu kwa ufasaha bado ni changamoto kwetu”alisema Feruz
No comments:
Post a Comment