RAY C : SIJAACHA KUTUMIA DOZI YA METHADONE

”Mimi naendelea na Methadone, huu ni mwaka wa
pili nakaribia namaliza, kwaiyo naendelea vizuri, kila mwezi kuna ripoti
inatoka inaenda kwa mheshimiwa na vipimo vyangu kila mwezi, nafanyiwa
vipimo, nafanyiwa counselling…katika wagonjwa ambao wanaoendelea vizuri
na Methadone”, alisema Ray c kwenye mahojiano na hot 255 ya Clouds fm.
Aidha mwanamuziki huyo amesema wanampango wa kuendelea na
projekti ya maskani kwa maskani kupitia mradi wake wa Ray C Foundation
na wanategemea kwenda mikoani ila kwa sasa wanajaribu kutafuta
wadhamini.
”Tunaplan ya kuendelea na projekti ya maskani kwa
maskani na tunategemea kwenda mikoani pia ila tunajipanga tuweze kuongea
na wadhamini, kwa sababu kwa nguvu zetu sisi wenyewe hatuwezi kuwafikia
watanzania wengi, kwaiyo tunachofanya tunajaribu kuongea na mashirika
mbalimbali”, alisema Ray C
No comments:
Post a Comment