RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI AMBULANCE KITUO CHA AFYA CHALINZE
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (katikati) akikabidhi gari
jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance), kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo,Dk. Mastidia Rutaihwa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chalinze,
katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jioni hii.
Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk. Bamba
Victor na Diwani wa Kata ya Bwilingu, Nasa Karama. (PICHA ZOTE NA
RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Muumini
wa Dini ya Kikiristo, Heema Said akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa
Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete 9aliyevaa koti kushoto) alipokabidhi
ambulance hiyo. Ridhiwani alisema kuwa yeye hivi sasa ni mbunge wa
vyama vyote jimbo humo hivyo ambulance aliyoitoa itoe huduma kwa wakazi
wote wa jimbo hilo bila kubagua watu kutokana na itikadi zao. Pia
aliuasa uongozi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanatunza vizuri gari hilo.
Dok
Rtaihwa akimkabidhi ufunguo wa gari hilo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya
cha Chalinze, Dk.Victor baada ambulance hiyo kukabidhiwa na Mbunge
Ridhiwani.
Dk. Victor akitoa shukurani kwa Mbunge Ridhiwani kwa msaada huo wa ambulance.
No comments:
Post a Comment