Header Ads

MBUNGE WA JIMBO LA MOROGOGO MJINI MH ABOOD AMWAGA MISAADA KATA YA BIGWA MOROGORO



 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akijibu Hoja Mbalimbali Kuhusu kero Zinazowakabili wakazi wa Kata ya Bigwa Katika Ziara yake ya Kutembelea Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Abood Aliata nafasi ya Kuongea na wakazi wa Mitaa wa Mitaa Mbalimbali inayounda Kata ya Bigwa.Mh Abood alijibu na Kutatua Kero Mbalimbali zinazowakabili wakazi wa Kata Hiyo.Mbunge Huyo alitoa Majibu Kuhusu Kero ya Umeme, Maji ,Barabara na Nyinginezo.Pia Mh Abood alitoa Misaada Mbalimbali iliyogarimu zaidi ya Milioni 20 Katika Kata ya Bigwa.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood akiwa kwenye banda la Mama Lishe maarufu Kama Mama Ntilie Ili Kujionea na kujua  Changamoto Zinazowakabili wamama hao katika kazi yao Hiyo wakati wa Ziara yake ya Kutembelea Kata ya Bigwa Jimbo la Morogoro Mjini
Baadhi ya Misaada aliyotoa Mbunge huyo kwa Wakazi wa Kata ya Bigwa.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akikabidhi vifaa Mbalimbali kwa Vikundi vya wakina Mama wanaojihusisha na Shuguli za Mama Lishe Katika Mitaa ya Vituli, Bomela, Korogozo,Mungi, na Mgolole Iliyopo Kata ya Bigwa.

No comments:

Powered by Blogger.