RIDHIWANI KIKWETE AAHIDI KUTATUA TATIZO LA UMEME, MAJI KIWANGWA,CHALINZE
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia), akipata maelezo kutoka
kwa Msimamizi wa ujenzi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ, Aloyce Mayunga
(kushoto) alipokwenda kukagua ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya
Kiwangwa wakati wa ziara ya kikazi ya katika Kata ya Kiwangwa, wilayani
Chalinze, Pwani leo.Aliwataka wajenzi hao kujenga maabara hayo kwa
kuzingatia viwango. Katikati ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya
ya Bagamoyo, Saleh Mpimbwi.
Ridhiwani
Kikwete akizungumza na wakandarasi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ
wanaojenga maabara ya Shule ya Sekondari ya Kiwangwa wakati wa ziara ya
kuagua miradi ya maendeleo na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa
mbunge miezi sita iliyopita. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA
MATUKIO BLOG
Ridhiwani
akinyoosha juu kadi ya Chadema aliyokabidhiwa na aliyekuwa Mwenyekiti
wa Chadema Kijiji cha Masugulu ambaye amehamia CCM katika mkutano wa
hadhara katika Kijiji cha Mwitemo Kata ya Kiwangwa leo
Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kijiji cha Mwitemo
Sehemu
ya akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani Kikwete
akihutubia katika Kitongoji cha Magogoni, Kijiji cha Msinune, Kata ya
Kiwangwa.
Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Msinune, Kata ya Kiwangwa.
No comments:
Post a Comment