CCM YALAANI VIKALI VURUGU ZILIZOFANYWA NA WAFUASI WA CHADEMA NA CUF KWA VIONGOZI WAO WA SERIKALI ZA MITAA.

Kamati Kuu
ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakutana Zanzibar
Januari 13, kwa kikao cha kawaida cha siku moja chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais
Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikao hicho
cha Kamati Kuu kitatanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu
kitakachofanyika Januari 10, jijini Dar es Salaam.
Wakati huo
huo CCM inalaani vikali vurugu zilizofanywa na wafuasi wa Chadema na CUF kwa
viongozi wetu wa serikali za mitaa katika maeneo kadhaa nchini ikiwemo mikoa ya
Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya.
Vurugu hizo
zilizosababisha baadhi ya viongozi wetu kujeruhiwa zimetokea katika mkoa wa
Mwanza ambapo Ndugu Christopher Mgeta kutoka Mtaa wa Ibungilo na Ndugu Pascal
Charles wa Mtaa wa Kitangiri A katika wilaya ya Ilemela walivamiwa na kupigwa
wakati wa kuwaapisha.
Katika mkoa
wa Dar es Salaam, Ndugu Sultan Jeta wa mtaa wa Ukwamani katika jimbo la Kawe
alifanyiwa fujo na wafuasi hao na Katika Mtaa wa Msisiri A kata ya Mwananyamala
katika jimbo la Kinondoni Ndugu Juma Mbena alipigwa na kuvunjwa mkono.
Katika
Manispaa ya Ilala, wafuasi hao wa vyama vya upinzani walifanya vurugu wakati wa
kuwaapisha viongozi hao wa serikali za mitaa wilayani humo na kusababisha zoezi
hilo kuahirishwa.
Mkoani Mbeya
vurugu za aina hiyo zimetokea katika wilaya za Kyela na Rungwe ambapo wilayani
Kyela zoezi la kuapisha viongozi wa serikali za mitaa lilishindika na
kuahirishwa kutokana na vurugu za kurushiwa mawe zilizofanywa na wafuasi wa
Chadema walioletwa kutoka katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Katika
kijiji cha Ilundo wilayani Rungwe wafuasi hao wa Chadema waliwapiga mawe
viongozi na wanachama wa CCM na baadae kufyeka mashamba yao ya migomba na
kusababisha vijana sita kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya
Rungwe kwa sababu ya hasira za kushindwa uchaguzi.
Vurugu
hizi ni mwendelezo wa tabia na mazoea ya vyama vya upinzani nchini kutoheshimu
na kufuata sheria na taratibu za nchi.
Tabia hizi si za kiungwana na ni uthibitisho wa kuharibikiwa na kufa kwa
vyama vya upinzani nchini. Mara zote
wamekuwa wakikataliwa na wananchi kwa kura, wao hukataa uamuzi huo wa wananchi
kwa kufanya fujo na vitimbi. Asiye kubali kushindwa si mshindani. Vurugu hizi sasa inatosha.
Imetolewa
na:-
Nape
Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
09/01/2015
09/01/2015
No comments:
Post a Comment