KIKUNDI CHA VIJANA WAJIITAO PANYA ROAD WAFUNGA MITAA NA KUZUA TAFRANI KUBWA JIJINI DAR

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar,Kamanda Kova akitoa ufafanuzi wa habari za taharuki katika vyombo vya habari hususani televisheni,kuhusiana na sakata la kundi la Vijana wajiitao Panya Road,amesema suala hilo lilikuwa dogo,lakini baadhi ya watu wamelikuza na kupelekea hofu kubwa kwa Wananchi ''Jiji mpaka sasa liko salama na wananchi watulie wasiwe na hofu kwa sababu jeshi la Polisi liko imara kuhakikisha amani inakuwepo ya kutosha,na hao vijana hawawezi kulishinda Jeshi la Polisi'',alisema.Alisema Wananchi waondoe hofu waendelee na shughuli zao kama kawaida.


Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa vijana hao waitwao Panya Road wameibuka na kufanya uhalifu huo mara baada ya tukio la Mwenzao mmoja kudaiwa kuuwawa na Polisi.
Aidha Chanzo hicho kimebainisha kuwa baada ya taarifa kusambaa kwa haraka,kimeeleza kuwa Jeshi la Polisi limeingia kazini kuwasaka watuhumiwa hao walioibua tafrani kubwa usiku huu.
Wadau tutazidi kuwaletea taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana.
No comments:
Post a Comment