DKT. KIGODA AZINDUA BODI YA UONGOZI YA CHUO CHA CBE LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Waziri
wa Viwanda na
Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Chuo
cha CBE na menejimenti ya chuo hicho kabla ya kuzindua rasmi Bodi mpya
ya uongozi ya chuo hicho leo.

Waziri
wa Viwanda na
Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) akimkabidhi mwongozo wa utendaji
kazi Mwenyekiti wa Bodi iliyoteuliwa ya uongozi wa Chuo cha Elimu ya
Biashara, Prof. Mathew Luhanga (kushoto) leo jijini Dar es salaam.

Waziri
wa Viwanda na
Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (katikati)
akizungumza jambo na viongozi na wajumbe wa Bodi mpya ya uongozi ya
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) iliyoteuliwa alipokuwa akitembelea
maeneo mbalimbali ya chuo hicho leo jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel
Mjema akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi Prof. Eleuther Mwageni na
Prof. Mathew Luhanga ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya CBE
(kulia).

Mkuu
wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema (kushoto)
akimwonesha Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda baadhi
ya maeneo ya chuo yaliyokuwa yamevamiwa na watu na kujengwa majengo
yakiwa wazi baada ya kubomolewa kufuatia uongozi wa chuo hicho kuendelea
na juhudi za kuyarudisha maeneo yote yaliyokaliwa kinyume cha sheria
chini ya umiliki wa chuo.

Waziri
wa Viwanda na
Biashara, Dkt. Abdallah (katikati)Kigoda akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha CBE na Menejimenti ya CBE leo
jijini Dar es salaam.

Waziri
wa Viwanda na
Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda akisalimiana na viongozi na wafanyakazi
wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam alipowasili
chuoni hapo kuzindua Bodi mpya ya uongozi ya Chuo hicho leo.Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
No comments:
Post a Comment