WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA KUWA MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI WA ALBAMU ‘USILIE’ DESEMBA 7, 2014

Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto (kulia).
WAZIRI
MKUU, Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu
‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7, mwaka huu.
Akizungumza
Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa
kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto, alisema hafla hiyo itafanyika
kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Uwanja wa Sabasaba, Dar es Salaam. Mbali ya uzinduzi huo Misheto alisema pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.

Aliwataja
waimbaji wa injili ambao watakuwepo siku hiyo kuwa ni Leah Mudy, AIC
(T) Vijana Chang’ombe, Accasia Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na
Frank Hume kutoka Boston nchini Marekani watatumbuiza.
Uzinduzi
huu umeratibiwa na Misheto Promotion, ambapo kabla ya uzinduzi huo
kutafanyika huduma za bila malipo za kiafya na kitabibu kutoka kwa
madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, ambayo yamekuwa yakiikabili
jamii.
Misheto
ameyataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari na mengineyo
ambapo huduma hiyo itatolewa na madaktari bingwa nchini. Picha zote na
Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
“Huduma
hii itaanza saa mbili asubuhi na itatolewa bure, ikiwemo ushauri na kwa
wale ambao wataweza kutibika watatibiwa, ila ambao watakuwa kesi zao
zimekuwa ni kubwa zaidi watapewa ushauri wa bure wa kuendelea na
matibabu katika hospitali kubwa na hakutakuwa na kiingilio," alisema
Misheto.
No comments:
Post a Comment