KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AMALIZA ZIARA YAKE NEWALA, LEO YUKO TANDAHIMBA

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la
Newala Kepteni Goerge Mkuchika wakati wa mapokezi wilayani Newala.

Wafanyakazi
wakibangua korosho kwenye kiwanda cha Micronix Newala ambacho
kilitembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo
kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoani Mtwara

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchagua korosho na
kuzitenga kutokana na ubora wa madaraja kwenye kiwanda cha Micronix
kilichopo Newala mkoani Mtwara.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)akishiriki kusuka nondo
pamoja na mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni George Mkuchika kwenye
ujenzi wa tenk la maji Kilidu wilayani Newala mkoa wa Mtwara.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua kituo cha afya cha Mkwedu
wilayani Newala ikiwa sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya CCM.

Jengo la Kituo cha Afya Mkwedu wilaya ya Newala.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Newala kwenye
viwanja vya Mahakama ya Mwanzo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa
Serikali lazima itafute namna ya kuhakikisha uzalishaji wa korosho wote
unafanyika nchini kwa kujenga viwanda vya kutosha vya korosho.
No comments:
Post a Comment