Header Ads

mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa watia fora,mamia wajitokeza

  Wananchi wakiwa katika foleni ya kuingia katika ukumbi wa mdahalo.
   Mwanaharakati wa mambo ya vijana Humphrey Polepole na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba akzungumza katika mdahalo huo.
   Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanyika jijini Dar es Salaam.Picha zote: Francis Dande
---
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema mambo yanayotokea sasa nchini, kama viongozi kuwa na akaunti nje ya nchi na kudai ni ‘vijisenti’, Serikali kuingia mikataba yenye utata isiyohojiwa popote ni matokeo ya nchi kuwa na Katiba yenye maswali mengi kuliko majibu.

Akizungumza katika mdahalo wa Katiba uliokuwa na mvuto wa aina yake kwa watu kushangilia kila mjumbe aliyakuwa anazungumza ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba huku akitumia zaidi mifano alisema mambo hayo yanaweza kuendelea kwa sababu hata Katiba Inayopendekezwa pia ‘imeyabariki’.

No comments:

Powered by Blogger.