MHE. KAMANI AZINDUA MRADI WA UFUGAJI WA SAMAKI NDANI YA ZIWA VICTORIA
Mgeni
Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya
Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa
Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia
mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John
Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.
Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani
akipandikiza vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi
unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule
cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki
kwenye vizimba.
Picha
ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga
vya samaki. Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya
Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF), Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa
Victoria, umekuwa ukitekelezwa pia na wenzetu wa Kenya na Uganda ambao
wamepiga hatua kubwa.
No comments:
Post a Comment