Serikali yatumia zaidi ya Bilioni 16 kujenga Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (the law school of Tanzania).
Afisa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law
School) Bi. Scholastica Njozi akiwaeleza jambo waandishi wa habari(hawapo
pichani) wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole.
Afisa Habari wa Wizara
ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole akiwaleza waandishi wa habari lengo la
uanzishwaji wa Taasisi ya Mafunzo ya Vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza
ya sheria ikiwa ni kuwaongezea ujuzi na stadi za kazi kwa ajili ya kutoa huduma
bora na yenye tija ka wananchi, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo
leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa
Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi.
Scholastica Njozi.
Mwanafunzi wa Taasisi
ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bw. Edwin Rwekaza
akiwaleza waaandishi wa habari kuhusu msisitizo unaotolewa na Taasisi hiyo
katika mafunzo kwa vitendo ili kuwaongezea ujuzi katika utekelazaji wa majukumu
pindi watakapo hitimu, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya
Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.
Mhadhiri wa Taasisi ya
Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Emil Lukiko akiwaeleza
jambo waandishi wa habari (Hawapo pichani) , wakati wa ziara iliyofanywa kwenye
Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law
School) Bi. Scholastica Njozi.
Mkuu wa Kitengo cha Mitihani wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Ipyana Mwaikambo akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani), Kuhusu idadi ya wanafunzi waliodahiliwa toka Taasisi hiyo imeanzishwa ambapo alisema zaidi ya wanafunzi 4000 wameshadahiliwa mpaka sasa, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.
Jengo
la Kufundishia(Teaching Block) katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Tanzania (Law School) lenye vyumba 2 vya mihadhara(lecture rooms)
vyenye uwezo wa kuingiza wanafunzi 460 kila chumba, vyumba 72 vya semina
Jengo
la Mahakama ya kujifunzia (Teaching Court) lililopo katika Taasisi ya Mafunzo
ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) litalofungwa Video Link ili
wanafunzi waweze kujionea moja kwa moja namna kesi zinavyoendeshwa
Muonekano
wa ndani wa Chumba cha Mahakama katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Tanzania (Law School)
Muonekano
wa ndani wa chumba mihadhara(lecture rooms)
(Picha na Hassan Silayo- MAELEZO).
No comments:
Post a Comment