MAREKANI YAJIUNGA NA MUUNGANIKO WA KIMATAIFA WA MAPAMBANO NDHIDI YA UHALIFU MTANDAO
Maswala
ya udukuzi yameendelea kushika kasi katika maeneo mbali mbali
ulimwenguni ambapo mataifa mbali mbali yameamua kuunganisha nguvu ya
pamoja kupambana na uhalifu mtandao. Katika "UCHAMBUZI" nilio
uandikia nilibainisha umuhimu wa kupata chombo kimoja chenye jukumu la
kupambana na uhalifu mtandao ambacho kitatoa nguvu kubwa ili kuweza
kukabiliana na hali mbaya ya uhalifu mtandao hivi sasa.
Kundi
jipya lenye makao yake barani ulaya linalounganisha pamoja nchi
wanachama wa bara ulaya pamoja na Canada, Colombia, Australia na
marekani limedhamiria kuunganisha mataifa mengine na kuhakiki maswala
mbali mbali yahusuyo usalama mtandao yanafanyiwa kazi ipasavyo.
Kwa
wafatiliaji wa habari za maswala ya usalama mitandao watakua wamepata
kuona taarifa mbali mbali za hivi karibuni zenye kuonyesha ukuaji wa
kasi wa uhalifu mtandao ambapo umetabiriwa kushika kasi zaidi kadri muda
unavyo zidi kwenda ambapo uhalifu mwingi wa sasa unategemewa kuhamia
katika mitandao.
Katika
andiko la naibu mkurugenzi wa chombo cha uingereza kinacho shughulikia
maswala ya uhalifu mtandao pamoja na kiongozi wa kundi jipya la
muunganiko wa nchi la kukabiliana na uhalifu mtandao kama inavyo someka "HAPA" wame
elezea ukuaji wa changamoto mbali mbali kwa vyombo vya usalama katika
mataifa mengi na kusisitiza kuna umuhimu mkubwa wa kuunganisha nguvu za
pamoja ili kuweza kufanikiwa katika vita dhidi ya uhalifu mtandao.
J-CAT
imedhamiria kuzileta pamoja nchi wanachama pamoja na mataifa mengine
yatakayo onyesha utayari ili kuweza kukabiliana kwa pamoja dhidi ya
uhalifu mtandao ambapo matumaini makubwa yatakua ni kukusanya taarifa za
kiuhalifu kutoka katika makampuni ya serikali na binafsi ili kubaini
aina za uhalifu na kujua maeneo athirika zaidi ili kuweza kuunganisha
nguvu. Nchi zaidi zitaenelea kushirikishwa baada ya majaribio ya mpango
huu wa kuunganisha nguvu kuweza kufikia pazuri.
Aidha, Chombo cha upelelezi cha Marekani (FBI) kupitia taarifa inayosomeka "HAPA" imebainisha
kulipa kipaumbele cha juu swala la mapambano dhidi ya uhalifu mtandao
kutokana na kilicho zungumzwa na mkurugenzi wake ya kuwa nchi hiyo
tayari imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na wahalifu wanao onekana
na kwa sasa wahalifu mtandao kua ndio changamoto yake kubwa na hivyo
wameazimia kuanza mapambano na uhalifu huo.
Kwa
upande mwingine katika mkutano mkuu wa maswala ya usalama mtandao wa
mwisho wa mwaka ambapo nimeteuliwa kuwa katika panel ya washauri mada
zinazotegemewa kujadiliwa na wataalam kutoka maeneo yote duniani ni
pamoja na kutafuta njia rafiki ya kufikiwa kwa malengo ya kuunganisha
hasa bara la afrika kuweza kuwa na njia ya pamoja ya kupambana na
uhalifu mtandao huku maswala ya kisheria za kimtandao yanavyo sumbua mataifa mbali mbali nini utatuzi wake.
Panategemewa
kupatikana taarifa kamili ya mkutano huo mapema ili watanzania ( wenye
ufahamu wa maswala ya usalama mtandao) nao waweze kushiriki.
No comments:
Post a Comment