KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ZIARANI HANDENI,AZUNGUMZA NA WANANCHI NA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI MBALIMBALI
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya
Kwaluguru wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya
maabara katika shule ya sekondari Kwaluguru wilayani Handeni.
Wananchi
wa kata ya Kwaluguru wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma
Kinana wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za
masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Kwaluguru ambapo vyumba 83
vya maabara vinajengwa wilayani Handeni.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege kwenye moja
ya vumba vya maabara za shule ya sekondari Kwaluguru.
Mbunge
wa Jimbo la Handeni Dk. Abdallah Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda
na Biashara akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vyumba vya maabara
vya sekondari ya Kwaluguru.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiujenzi wa ofisi ya CCM
Tawi la Kweinjugo kata ya Kwaluguru wilaya ya Handeni
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicheza ngoma ya asili ya wazigua .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika ambapo aliwaambia wajifunze kupima mambo ya viongozi wa siasa wasije wakaingizwa kwenye matatizo bila kutarajia kwani wapo zaidi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na si ya wananchi ndio maana wanadiriki kutangaza maandamano wakati wao wenyewe hawapo wameenda nje ya nchi kupumzika.
No comments:
Post a Comment