DK. TIZEBA ATOA MISAADA KWA WAHANGA WA MOTO JIMBONI KWAKE
Naibu
Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk
Charles Tizeba akipanda boti kuelekea kisiwa cha Nyamango kulikotokea
ajali ya moto kwa ajili ya kukabidhi misaada.
Na Daniel Makaka, Sengerema.
NAIBU
Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles
Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya moto na nyumba
zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha Nyamango kijiji cha
Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa
Mwanza.
Misaada
aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia tatu na Magunia manne ya
Unga wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote vyenye thamani ya shilingi
million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa kwa kaya hamsini na moja
ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu.
Akikabidhi
misaada hiyo Dk Tizeba aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo
inawafikia walengwa na siyo vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao
hao kutumia misaada kwa lengo la kuwasaidia wakati kamati ya maafa
wilaya ya Sengerema ikiwa bado inaendelea kufanya tathimini il iione
namna ya kuwasaidia.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk
Charles Tizeba akiwa ndani ya boti kuelekea kukabidhi misaada katika
kisiwa cha Nyamango jimboni kwake.
Serikali
itaendelea kusaidia kadri iwezavyo si kwamba watapewa fidia bali ni
misaada tu.Awali Katibu wa kamati ya maafa wilaya Sengerema Bw. Benard
Myatilo akitoa taarifa ya wahanga wa tukio hilo alisema kuwa matukio
hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo Septemba 19 majira ya saa nane
usiku kaya 40 ziliteketea kwa moto na chanzo cha moto huo ni kulipuka
kwa Kibatari ndani ya nyumba na tukio la pili kaya 11 kuezuliwa na mvua
ilyoambatana na upepo likiwemo jengo la kanisa Katoliki kisiwani humo.
Pia
alisema kati ya wahanga hao hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio
hayo licha mali zote zlizokuwemo kuteketea ambapo hadi sasa kaya saba
hazina mahali pakuishi huku zilizobaki zikihifadhiwa na baadhi ndugu na
jamaa wanaoishi katika kisiwa hicho.
Muonekano wa baadhi ya nyumba zilizoteketea kwa moto katika kisiwa cha Nyamango wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.
Kanisa la Roman Katoliki katika kisiwa cha Nyamango lililoezuliwa na upepo ulioambatana na mvua.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles
Tizeba (mwenye suti ya kijivu) akikabidhi misaada ya mablanketi 300 kwa
Mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba, Deus Bitulo (kulia kwa naibu waziri)
huku Mwenyekiti wa CCM tawi la Nyamango, Japhet Kafula akishuhudia
tukio hilo
No comments:
Post a Comment