MATUKIO ZAIDI YA POLISI WALIPOSHAMBULIA WAANDISHI WA HABARI WAKITAWANYA WAFUASI WA CHADEMA
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akiwasili
kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema leo asubuhi tayari
kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama
hicho hivi katibuni,kuwa watafanya maandamano nchini nzima bila kikomo.
Kauli hiyo ya makamu wa rais imeshindwa kutekelezwa kutokana na tukio lililotokea majira ya saa 5 na dk 15 asubuhi wàkati mwenyekiti wa chadema taifa Mhe. Freeman Mbowe alipowasili makao makuu na askari wa polisi kutaka kuzuia gari alilopanda kuingia ndani ya lango kuu pamoja na waandishi wa habari na watu wengine kuamriwa kuondoka katika eneo hilo agizo lililopingwa na waandishi wa habari na baadhi ya wanasheria wa Chadema.
Kufuatia na kutolewa kwa ilani hiyo jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia-FFU- kilianza kupiga waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wananchi huku wengine wakikimbia kuhofu vipigo toka kwa askari hao ambapo baaadhi ya waandishi walioumizwa sehemu mbalimbali ya mihili yao.
Akiwatangazia wafuasi waliokuwa wakikataa kuondoka katika maeneo hayo mwanasheria wa chadema mhe. Tundu lissu licha ya kuwahakikishia kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa Mhe. Freeman Mbowe yuko salama amewataka kuondoka katika eneo hilo na kurudi majumbani ili kuepusha vurugu na misongamano ambayo ingeweza kusababisha matatizo zaidi.
Aidha ITV imeshuhudia mwenyekiti wa Chadema taifa Mhe Freeman Mbowe akitoka makao makuu ya jeshi la polisi akisindikizwa na ulizni mkali wa jeshi la polisi kuelekea katika ofisi za makao makuu ya chama hicho baada ya kukamilika kwa taratibu za kipolisi.
Wafuasi wa Chadema wakimsindikiza mwenyekiti wao Freeman Mbowe kuelekea Makao makuu ya jeshi la polisi
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika akizungumza na waandishi wa
habari waliokuwepo kwenye eneo la makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya
kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiani katika ya Mwenyekiti wa
Chama hicho na Jeshi la Polisi.
Makamu
Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa Chama,Wakili
Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la Polisi.
Mwenyekiti
wa Chama cha DP, Christopher Mtikila akihojiwa na askari Polisi,
alipowasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa kutumia
usafiri wa bajaji, ambako Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alihojiwa
na Polisi.
Chanzo : ITV
No comments:
Post a Comment