JOPO LA MAJAJI KWA AJILI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YAFANYA ZIARA KATIKA MIGODI YA BULYANHULU NA BUZWAGI
Mkurugenzi Mtendaji
wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Gold
Mine Bw. Peter Burger ( wa kwanza kushoto) akizungumza na jopo la majajaji na sekretarieti iliyotembelea mgodi huo kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Ibanza Bw. Dions Kagiye
(katikati) akizungumza na baadhi ya
majaji waliotembelea shule hiyo inayofadhiliwa na mgodi wa Bulyanhulu Gold Mine
kwa ajili ya kuifanyia tathmini
Mmoja wa majaji Dkt.
Yohana Mtoni (kushoto) akimsaidia mmoja wa watoto waliofika katika kisima cha
maji cha Ilogi kuvuta maji. Kisima hicho kinafadhiliwa na mgodi wa Bulyanhulu
Meneja Mahusiano wa
Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga Bi. Dorothy Bikurakule ( wa kwanza kulia mbele) akiongoza jopo la majaji na
sekretarieti kutembelea kituo cha afya cha Mwendakulima kinachofadhiliwa na
mgodi huo.
Meneja Mahusiano wa
Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga Bi. Dorothy Bikurakule (katikati) akielezea mchango wa
mgodi huo katika uwezeshaji wa kikundi
cha vijana cha ufyatuaji wa matofali cha Mwendakulima.
Mwalimu Mkuu wa Shule
ya Sekondari ya Mwendakulima Bi. Diana Kuboja akielezea mchango wa mgodi wa
Buzwagi Gold Mine katika ujenzi wa shule hiyo
kwa majaji na sekretarieti
iliyotembelea shule hiyo kwa ajili ya kufanya
tathmini.
No comments:
Post a Comment