WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA) KANDA YA DODOMA INAKABILIWA NA UFINYU WA ENEO LA KUHIFADHIA MAZAO MSIMU HUU WA UNUNUZI WA MAZAO
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua shughuli za ufungashaji
mahindi na Mtama kwenye magunia tayari kwa kuhifadhiwa kwenye maghala wakati alipotembelea kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma.
Wakinamama kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakipeta mahindi na kuyaondoa uchafu tayari kwa ajili ya kuyafungasha kwenye magunia na kuyahifadhi ghalani, mahindi hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali.
Moja ya maghala ya NFRA Kanda ya Dodoma ambayo yamejaa mahindi na Mtama na hivyo kuhitaji maeneo/maghala mengine zaidi ya kuhifadhia mazao.
Gari iliyobeba mahindi ikipima uzito ili kupeleka mahindi hayo kuhifadhiwa kwenye maghala kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao hayo.
Baadhi ya Magari ya mizigo yakipakua mahindi na mtama kwenye kituo cha (NFRA) Kanda ya Dodoma.
Magari yaliyobeba mahindi na mtama yakiwa kwenye foleni nje ya kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakisubiri kuuza mazao hayo kwa wakala huyo wa serikali kama walivyokutwa kituoni hapo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja naC baadhi ya wanachama wa vyama mbalimbali vya ushirika vya kilimo vilivyoleta mazao kuuza kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, mapema jana wakati ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mazao kituoni hapo.
No comments:
Post a Comment