TASAF YAWAFUNDA WATAALAM WA KISEKTA JUU YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI-PSSN
Mkurugenzi
mtendaji wa TASAF, bwana Ladislaus Mwamanga amesema utekelezaji wa Mpango wa
kunusuru kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF
utasisimua shughuli za maendeleo kwenye maeneo mbalimbali ya nchi ambako
utatekelezwa na hivyo kuwa chachu ya maendeleo na kuondoa kero zinazowakabili wananchi hususani
suala la umasikini.
Bwana
Mwamanga amesema hayo jiji Dar es salaam alipofungua warsha ya wataalamu wa kisekta kutoka
Tanzania Bara na Zanzibar ambao sekta zao zinahusika kwa namna moja au nyingine
katika utekelezaji wa shughuli za TASAF kwenye maeneo yao.
Mkurugenzi
mtendaji huyo wa TASAF amesema kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya
masikini umeanza kutekelezwa kwa mafanikio ambapo mwelekeo umeonyesha kuwa
maeneo ambako Mpango huo umefanyiwa majaribio kumekuwa na mafanikio ya kujivunia
hususani katika sekta za Elimu, Afya, na hata Lishe kwa kaya ambazo hapo awali
hazikuwa na uhakika wa kupata lishe.
Hata
hivyo, bwana Mwamanga amewataka wataalamu hao wa kisekta kutumia utaalamu wao
ipasavyo ili waweze kuielewa dhana nzima ya Mpango wa kunusuru kaya masikini na
kuhakikisha kuwa wanawawezesha wananchi hususani walioko katika kaya masikini
ili waweze kuondokana na umasikini.
Mkurugenzi
huyo mtendaji wa TASAF pia ametaka mkakati maalum uwekwe ili kuhakikisha kuwa
huduma muhimu hususani za upatikanaji wa elimu na Afya unakuwapo ili walengwa wa mpango huo waweze kunufaika
nazo.
Zifuatazo ni
picha za ufunguzi wa warsha hiyo ya wataalamu wa kisekta iliyofanyika leo katika
hoteli ya Golden Jubelee jijijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus
Mwamanga (aliyesimama) akifungua warsha ya wataalam wa Kisekta (hawapo pichani) jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi
wa Miradi wa TASAF Bwana Amadeus Kamagenge (aliyesimama)akitoa maelezo ya
utangulizi katika warsha ya wataalamu wa kisekta jijini Dar es salaam katikati ni Mkurugenzi
mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga na
kushoto kwake ni mkurugenzi wa uratibu wa TASAF
Alphonse Kyariga.
Mkurugnezi
wa uratibu wa shughuli za Muungano katika Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Bwana Issan Ibrahim Mohmond (aliyevaa koti )akimsikiliza mkurugenzi mtendaji wa
TASAF, Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) alipofungua warsha ya wataalam wa kisekta
jijijin Dar es salaam mbele yake ni
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa TASAF Bwana Christopher Sanga.
Baadhi
ya washiriki wa warsha ya wataalamu wa Kisekta wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
wa warsha ya wataalam wa kisekta iliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wa TASAF
Ladislaus Mwamanga(hayupo pichani).
Baadhi
ya washiriki wa warsha ya wataalamu wa Kisekta wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
wa warsha ya wataalam wa kisekta iliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wa TASAF
Ladislaus Mwamanga(hayupo pichani).
Mtaalamu
wa teknolojia ya habari na mawasiliano ICT wa TASAF Bwana Peter Luanda(wa
kwanza kushoto)na meneja wa uhawilishaji
wa fedha Bwana Omar Malilo (mwenye miwani katikati)wakiwa katika warsha ya
wataalamu wa kisekta iliyoandaliwa na TASAF jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (aliyeketi katikati )akiwa katika picha
ya pamoja na washiriki wa warsha ya wataalam wa kisekta iliyoandaliwa na kwa lengo la kuwaelewesha
namna ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini nchini unaoratibiwa na
Mfukowa Maendeleo ya Jamii TASAF.
No comments:
Post a Comment