Tanzania yatimiza miaka 50 ya Muungano
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Sherehe
za kuhadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyozaa
nchi ya Tanzania zimefanyika leo mjini Dar es Salaam na kupambwa kwa
maonyesho mbali mbali ya kijeshi pamoja na halaiki zilizoandaliwa na
watoto.
Marais
wanne wa nchi za Afrika Afrika Mashariki akiwemo Yoweri Museveni wa
Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi ni
miongoni mwa marais waliohudhuria sherehe hizo.
Wengine
ni Rais Joyce Banda wa Malawi, Mfalme Mswati III wa Swaziland, mfalme
Letsie III wa Lesoto Makamu wa Rais wa Nigeria Mohammed Sambo, Makamu wa
Rais wa Zambia Guy Scott, Waziri Mkuu wa Rwanda Piere Habumurenyi,
Waziri Mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai
Kibaki.
Katika maadhimisho yao pia kulikuwa na maonyesho ya silaha mbali mbali za kivita zikiwemo ndege za kivita pamoja na za kiraia.
Hata
hivyo kilichovutia zaidi ni kikosi cha makomandoo wa jeshi la Tanzania
ambao walionyesha umahiri wao kupambana na adui bila kutumia silaha na
kuvunja vitu vigumu kwa kutumia kichwa pamoja na mikono.
Onyesho
jingine lililotia fora ni askari wa miamvuli ambao waliruka kutoka
kwenye ndege kwa kutumia miavuli na kutua katika uwanja wa sherehe.
No comments:
Post a Comment