PICHA : WASANII WA MUZIKI TANZANIA WAFANYA VIDEO YA WIMBO WA KUDUMISHA MUUNGANO
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya muungano, Wasanii wa fani ya muziki Tanzania wameungana kwa pamoja na kufanya video ya wimbo wenye dhima ya kudumisha umoja na mshikamano wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ambao ulitiwa saini na waasisi wa Taifa letu, Mzee Julius Kambarage Nyerere na Mzee Aman Abeid Karume.
Kama ilivyo miaka ya muungano na ndivyo hivyo idadi ya wasanii walioshirikiana kwenye wimbo huku kila mmoja akiwa ametupia vazi la Taifa,. Wimbo huo umejumuisha wasanii wa Bongo Fleva, Taarabu, Dansi, Gospel na Raga.
No comments:
Post a Comment