MASHINDANO YA MBUNGE YAMALIZIKA
Mbunge Kabati
akikabidhi mipira kwa mratibu wa mashindano Rashid Bilo 'Shungu'
katika makabidhiano yaliyofanyika katika uwanjwa wa Ipogoro.
Mbunge kabati akifunga mashindano ya Rita Kabati Vijana Cup yaliyofanyika katika Kata ya Ruaha mjini Iringa
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati akionyesha uwezo wake
kisoka huku mkuu wa wilaya ya Kibonde Venance Mwamoto kulia akishangaa
utaalam wa mbunge huyo.
00000000 0000000 0000000
MASHINDANO YA MBUNGE
YAMALIZIKA
Na Denis Mlowe,Iringa
MASHINDANO ya kombe la mbunge yanayojulikana kwa
jina la ‘Rita Kabati Vijana Cup’ yanayodhaminiwa na mbunge wa Viti maalum kwa
tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Rita Kabati, yamefikia ukingoni juzi
katika kata ya Ruaha jimbo la Iringa mjini huku mbunge huyo akiahidi
makubwa kwa wanamichezo jimboni hapo ikiwa ni pamoja na kuifikisha
bungeni timu itakayofanya vema .
Akizungumza juzi wakati wa
fainali ya kombe hilo mchezo uliofanyika uwanja
wa shule ya Msingi Ipogolo na kuzikutanisha timu za Jamaica Fc na News
Boys ,Kabati alisema kuwa ameamua kuanzisha mashindano
mbali mbali ya soka kwa vijana kama njia ya kuinua soka katika
mji wa Iringa na vitongoji vyake.
Alisema kuwa mbali ya mashindano hayo kumalizika
anakusudia kuanzisha mashindano mengine ambayo mbali ya
mshindi kupewa zawadi mbali mbali bado timu bingwa
ataipeleka bungeni mjini Dodoma ili kutambulishwa na kuhudhuria kikao
kimojawapo cha bunge.
Kabati alisema kuwa katika ilani ya CCM
inasisitiza jinsi ambavyo itakavyoendeleza sera ya
michezo kwa vijana na tayari utekelezaji huo
umeanza katika mkoa wa Iringa na maeneo mbali mbali ya nchi.
Aongeza kuwa kama mbunge wa mkoa wa
Iringa atahakikisha vijana wanaanzishiwa mashindano ya mara kwa mara
ili kuwaepusha na vishawishi mbali mbali kama utumiaji wa madawa ya
kulevya pia kuifanya michezo
"Nina mpango wa kuendeleza
vijana kimichezo na ikiwezekana ligi kuu kuanzwa kuchezwa
mkoa wa Iringa iwapo timu zetu zitafanya vema katika mashindano
mbali mbali kama ilivyo mikoa mingine ambayo imeendelea kisoka
zaidi" alisema Kabati
Katika fainali hiyo
News Boys ilifanikiwa kuchukua ubingwa kwa kuwafunga Jamaica kwa penati 5 – 4
baada ya dk 90 kufungana goli moja kwa moja.
Katika
mechi hiyo wafungaji walikuwa Hasan Peng’e kwa upande wa Jamaica Fc
na Michael Kalinga kwa upande wa News Boys.
Kwa
upande wake mratibu wa mashindano hayo Katibu Mkuu wa Chama cha Soka
Manispaa ya Iringa, (IMFA) Rashid
Shungu alisema kuwa mbunge huyo ameonyesha jitihada kubwa
katika kuendeleza soka mjini Iringa na kumuomba kuendelea
zaidi kusaidia soka Iringa.
Shungu alisema mashindano hayo
yameleta chachu kubwa ya soka katika kata ya Ruaha ambapo
vijana wengi wamehamasika na kuonyesha uwezo wa hali ya
juu katika soka na kuwa lazima kuweka mkakati wa kudumu wa
kuendeleza vijana hao kisoka.
No comments:
Post a Comment