Header Ads

WANAHABARI IRINGA HOI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO MZEE WA MATUKIODAIMA AONGOZA


Mmiliki wa  mtanmdao huo mzee wa  matukiodaima kulia akipunga mkono sanjari na mwandishi wa Mjengwa Blog baada ya kuweka rekodi ya aina yake kwa  wanahabari Iringa kwa  kupanda mlima Kilimanjaro kutoka Getini hadi kituo cha kwanza cha Mandara kwa saa 1.45 badala ya masaa 3 kama ilivyokawaida huku mzee wa matukiodaima Bw Francis Godwin akishika nafasi ya kwanza kufika eneo hilo akifuatiwa  na Daniel Mbega kutoka Mjengwa blog na Abukarim Mshana kutoka radio QBRATEN huku baadhi ya  wanahabari kutoka Iringa wakishindwa kushuka na kulazimika kushushwa na  gari la  wagonjwa (AMBULENCE)(picha zote na Francis Godwin Blog)

Pamoja na kudai mlima kilimanjaro upo Kenya,hapa  wasnafunzi  kutoka nchini Kenya wakipanda mlima Kilimanjaro sanjari na  wanahabari Iringa kama  walivyonaswa na kamera ya matukiodaima ,kama mlima yungekuwa Kenya si  wangepanda mlima huu kupitia Kenya?
Vijana  waongoza  watalii katika mlima Kilimanjaro wakimsaidia kumshusha kutoka mlimani mmoja kati ya  watalii watano kutoka  nje ya Tanzanie aliyepoteza fahamu kwa  kupanda mlima huo kama walivyokutwa na kamera  ya matukiodaima wakiwa eneo la  kituo cha kwanza  cha MANDARA
 Baadhi ya  wanahabari kutoka mkoa  wa  Iringa wakiwa  ktk picha  kabla ya  kuanza  kupanda mlima Kilimanjaro
Katibu  wa  chama  cha  waandishi  wa  habari  mkoa  wa Iringa Bw. Francis Godwin ama mzee wa  matukiodaima wa pili kulia ,mwanahabari Abukarim Mshana  wa radio Qbra Ten Fm na mwandishi wa Mjengwa BLOG kushoto wakipongezana  na  watalii wa  nje  baada ya  kufanikiwa kuweka rekodi ya  kupandisha  mlima  huo kwa mwendo wa kukimbia na  kutumkia  saa 1 .45 kutoka  getini hadi  kituo cha kwanza cha MANDARA badala ya masaa matatu na  kushuka kwa  dakika 45

No comments:

Powered by Blogger.