Header Ads

TUTAELIMISHA UJINGA NA MARADHI-MDEE


1 (2)
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tanga Bi. Monica Kalani akitoa nasaha kwa washiriki wa mafunzo ya uaandaaji wa vipindi vya elimu kwa umma yaliyoendeshwa na TBC kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
2 (2)Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akitoa maelezo ya awali wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
3 (1)Mkurugenzi wa Huduma za Radio katika Shirika la Utangazaji  Tanzania Suzan Mungy akielezea namna mafunzo yalivyoendeshwa kwa washiriki hao.
4 (2)Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa mafunzo hayo.
5 (2)Mmoja wa washiriki kutoka kitengo cha Damu Salama Bw. Rajab Mwenda kipokea cheti cha kushiriki mafunzo ya uaandaji wa vipindi vya elimu kwa umma.
6 (1)Picha ya pamoja kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema unaelekeza nguvu zaidi katika kuelimisha umma kujikinga na maradhi, hususan yasiyoambukiza ili kupunguza maradhi hayo kwa wanachama na wananchi kwa ujumla lakini pia gharama za matibabu ambazo Mfuko unalipa kwa watoa huduma wanaotibu wanachama wake.
Akizungumza  katika mkutano wa waandaji wa vipindi vya elimu kwa umma kutoka katika Wizara na Taasisi mbalimbali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee aliyataja maradhi hayo kuwa ni pamoja na saratani, kisukari, shinikizo la damu na uzito uliokithiri ambayo yamekuwa yakiongezeka sana na kusababisha vifo miongoni mwa jamii.
“Magonjwa haya yanaongezeka kila kukicha na gharama za matibabu yake ni kubwa sana hivyo ni lazima sasa tuweke nguvu kubwa ya elimu inayohusu kujikinga na maradhi haya nah ii itawasaidia sana wananchi kujua namna ya kuepukana nayo,” alisema Bw. Mdee.
Aidha Bw. Mdee amesisitiza kuwa NHIF itaendelea kushirikiana na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika mafunzo ambayo yamekuwa yakiandaliwa na shirika hilo kwa waandaji wa vipindi ili yawe bora zaidi na manufaa kwa taasisi wanazofanyika kazi na Serikali kwa ujumla.
Kwa upande wa Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tanga Bi. Monica Kalani ambaye alifunga rasmi mafunzo hayo ya siku 10 alisisitiza umuhimu kwa watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa kutumia lugha fasaha katika kuwasilisha mada kwa wasikilizaji na watazamaji wa vipindi vyao.
Alisema watazamaji na wasikilizaji wa vipindi vya elimu kwa umma kupitia TBC 1 na TBC Taifa wanaimani kubwa na vyombo hivyo vya habari, kwa hiyo ni wajibu wa watayarishaji wa vipindi vinavyorushwa kupitia vyombo hivyo kutimiza matarajio ya wasikilizaji na watazamaji wao.
“Nyie ni kundi muhimu sana katika maeneo yenu ya kazi hivyo mafunzo haya kayatumieni vizuri ili yaoneshe matunda, wananchi wanahitaji sana elimu mbalimbali kupitia vipindi vya radio na televisheni,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vipindi vya Redio wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Bi. Suzan Mungi, ameipongeza NHIF kwa kuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa watayarishaji wa  vipindi vya elimu kwa umma.
“Tunaishukuru sana NHIF kwani mmewezesha kwa kiwango kikubwa kufanikiwa kwa mkutano huu na kwa ushirikiano mkubwa mlioutoa na kwa upande wetu kama TBC tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu ili elimu ama kazi mnazozifanya ziweze kutambulika kwa jamii,” alisema.
Mafunzo hayo ya siku kumi yalihitimishwa rasmi jana ambapo washiriki wa mafunzo hayo walitoka katika Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali nchini.

No comments:

Powered by Blogger.