Header Ads

Serikali imedhamiria kufufua vuguvugu la michezo nchini


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea vifaa mbali mbali vya michezo kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Hassan and Sons kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake Mohd Raza kusaidia mashindano ya Kombaini  za wanafunzi wa Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Baadhi ya vifaa na vyakula vilivyotolewa na Kampuni za Hassan and Sons, Zat pamoja Zanzibar Ocean View hapo Wizara ya Elimu Maziri kusaidia mashindano ya Kombaini za wanafunzi wa skuli za Zanzibar.

.
 Seti za Jezi tyofauti zilizotolewa na wafanyabiashara kwa ajili ya wanamichezo watakaoshiriki mashindano ya Kombani za Maskuli ya Zanzibar yanayotarajiwa kuanza rasmi tarehe 29 mwezi huu katika uwanja wa Uzini Wilaya ya Kati.

 Baadhi ya walimu wa skuli mbali mbali nchini walioshiriki hafla ya makabidhiyano ya vifaa mbali mbali vitakavyotumika kwa ajili ya mashindano ya Kombaini za Maskuli Nchini.

 Mwenyekiti Mtendajio wa Kampuni ya Hassan and Sons Mohd Raza  akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kutumika katika mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya mashindano ya kombe la Mapinduzi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi ambae pia ni Mwenyekiti wa BTMZ Ssharifa Khamis akitoa shukrani zake mara baada ya kupokea msaada wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya mashindano ya kombe la Mapinduzi.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  imedhamiria kufufua upya vugu vugu la michezo Nchini ili kuirejeshea hadhi yake Zanzibar katika Nyanja za Michezo Kimataifa.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo katika hafla fupi ya kukabidhiwa  vifaa vya michezo pamoja na vyakula kwa ajili ya washiriki wa mashindano ya Kombaini za wanafunzi za Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliyofanyika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 
Balozi Seif alisema  heshima ya Zanzibar  kimichezo lazima  iwepo kwa kuhakikisha  Vijana wanaandaliwa vyema Maskulini ambako ndiko kunakopatikana  vipaji vya michezo mbali mbali vinavyoweza kuirejeshea heshima yake Zanzibar.
 
Alifahamisha kwamba jamii popote pale hapa Nchini inahitajika kuongeza ari ya kuwaamsha vijana kwenye mitaa yao katika kupenda na hatimae kushiriki kwenye michezo tofauti kulingana na uwezo wa vijana wenyewe

No comments:

Powered by Blogger.