MISS TANZANIA 2013 HAPPINESS WATIMANYWA ALA KRISTMAS NA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA MGOLOLE MOROGORO.
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa (pichani), Leo amejumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro. Mrembo huo ameungana na warembo wengine wawili , akiwemo Miss Kanda ya Mashariki Missa Clara Pamoja Sabra Islam Miss Morogoro 2013 . Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa.Aliongozana na Wazazi wake pamoja na Ndugu jamaa na marafiki zake.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega Akiwa na Katibu wa Miss Tanzania Bosco Majaliwa leo awlipoongozana na Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Alipotembelea Kituo cha Kulea watoto Yatima cha Mgolole Kinachomilikiwa na Masista wa Moyo safi Wa Maria Cha Mkoani morogoro.
Watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha masista wa Moyo Mtakatifu wa Maria cha Mgolele mkoani Morogoro wakiwa katika Picha ya Pamoja leo walipopata Ugeni Kutoka kwa Miss tanzania Happiness Watimanywa Aliyeambatana na wakurugenzi wa Miss tanzania Pamoja na Wazazi wake ndugu na jamaa wake wa Karibu.
Ndugu na Marafiki wa Miss tanzania 2013 waliomsindikaza Happiness Watimanywa Alipotembelea kituo cha watoto yatima cha mjini Morogoro..
Picha na Habari kwa hisani ya shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment