KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA CHUNYA,KESHO NI MBARALI
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisogeza matofali kwa Nape Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kuyapandisha juu kwa ajili ya ujenzi wa
soko la Mulugo Market Mwambani lililopo katika ya kata Mwambani wakati
viongozi hao waliposhiriki ujenzi wa soko hilo linalojengwa na Mbunge wa
jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Mh.
Philip Mulugo katika kuwakwamua kiuchumi wananchi wa jimbo la Songwe
wilayani Chunya, Kinana amemaliza ziara yake katika wilaya hiyo na kesho
anaanza ziara katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya. (PICHA NA KIKOSI
KAZI CHA FULLSHANGWE-MKWAJUNI-CHUNYA)
Mkuu
wa wilaya ya Chunya Ndugu Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa
bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Maweni kata ya Mwambani
wilayani Chunya kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili
kutoka kulia wakati alipokagua ujenzi wa bweni hilo lililojengwa kwa
msaada wa Shirika la maendeleo la watu wa Japan (JAICA) kulia ni
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Ndugu Godfrey Zambi.
Abdulrahman
Kinana akipata maelezo kutokam kwa mkuu wa shule ya sekondari ya Maweni
wakati alipokagua ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba mbili
za walimu katika shule ya msingi ya Saza katika kata ya Saza Mkwajuni
Chunya, anayeshuhudia ni mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wafugaji katika kijiji cha Mteka kata ya Kapalala.
Wafugaji wa kijiji cha Mteka kata ya Kapalala wilayani Chunya wakimpokea kwa ushujaa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana huku wakiimba nyimbo za kumsifu wakati alipowasili katika kijiji hicho cha wafugaji.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Ndugu Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa
ajili ya kulnywesha mifugo yao lakini pia kutumia kwa shughuli za
kibinadamu kisima hicho kimefungwa mitambo inayovutamaji kwa kutumia
upepo Power Wind, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na
Uenezi na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Mh. Godfrey Zambi.
Kisima chenyewe ndiyo hiki.
wafugaji wakifurahia jambo wakati Kinana alipokuwa akiongea nao.
Abdulrahman Kinana akiuliza jambo wakati akikagua maradi huo katika eneo la matanki ya maji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Gegwa Luhende mara baada ya kuzindua mradi huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na wafugaji kuelekea eneo la kunweshea mifugo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiuliza jambo kutoka kwa injinia
wa idara ya maji Wilaya ya Chunya Bw Ndele Mengo wakati akikagua lambo
hilo la kunyweshea mifugo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, katikati Mbunge wa jimbo la
Songwe Mh. Philip Mulugo kulia na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa
na Uenezi wakila chakula kilichoandaliwa na jamii hiyo ya wafugaji kwa
ajili ya wageni.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa bweni la
wanafunzi katika shule ya sekondari ya Kapalala kata ya Kapalala ambalo
linajengwa na wakulima wa Tumbaku kupitia taaisis yao ya Chunya
Development Trust.
Mbunge
wa jimbo la Songwe Mh. Philip Mulugo kushoto na mkuu wa wilaya ya
Chunya Deodatus Kinawiro kulia wakishiriki kazi ya kusomba tofali katika
ujenzi wa bweni la shule ya sekondari ya Kapalala wilayani Chunya,
Mbunge
wa jimbo la Songwe Mh. Philip Mulugo akizungumza na wananchi wa Udinde
mahali ambapo ndipo alipozaliwa wakati wa mkutano wa hadhara leo.
Wananchi walipanda hata kwenye miti ili kumshuhudia katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Udinde.
Katibu wa CCM wilaya ya Chunya Braison Mwasimba aliyejejea CCM jana akiwapa ukweli wananchi wa kijiji cha Udinde.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubiwa wananchi wa kijiji cha Udinde Mkwajuni leo.
No comments:
Post a Comment