Home
Unlabelled
BAADHI YA WANAFAMILIA YA NELSON MANDELA WALALAMIKA KUTOALIKWA KATIKA MSIBA HUO KUTOKA NA HALI ZAO ZA MAISHA KUWA DUNI.
BAADHI YA WANAFAMILIA YA NELSON MANDELA WALALAMIKA KUTOALIKWA KATIKA MSIBA HUO KUTOKA NA HALI ZAO ZA MAISHA KUWA DUNI.
Pichani ni Mpwa wa late Nelson Mandela, Nokhaya Mkwedini ambaye ni mmoja wapo wa wanafamilia hiyo aliyetengwa kwa kutopewa mualiko wa kuhudhuria msiba huo.
Wakati nchi ya Afrika Kusini na Dunia kwa ujumla wakiomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, baadhi ya wana ukoo wa Mandela wameeleza kusikitishwa kwao kufuatia kutengwa na familia ya mzee Nelson Mandela kwa kutopewa mualiko kutokana na hali zao za kimaisha kuwa Duni.
akiongea na kituo kimoja cha habari nchini Afrika Kusini, Mpwa wa Nelson Mandela aliyejitambulisha kwa jina la okhaya Mkwedini alinukuliwa akisema kwamba mtu anayepaswa kulaumiwa ni mtoto wa kike wa kwanza wa Mandela anayeitwa Makaziwe(59) kutokana na kuwa na jukumu la kuwaalika wanaukoo hao kwenye shughuli hiyo ya msiba na hata mume wake alivyomwambia kuhusu habari za kwenda kwenye msiba nilimkatalia, mpwa huyo aliendelea kufunguka zaidi kwa kusema kwamba hawakuweza kupewa mualiko kutokana na hali zao za kimaisha kuwa Duni hivyo uwepo wao kwenye msiba huo ungekuwa kama vile kuiabisha familia ya mzee Mandela kutokana na viongozi wakubwa wa Dunia kuwepo , na kisha alimalizia kumalizia kwa kusema kwamba laiti kama marehemu Nelson Mandela angelifufuka kesho angehudhunishwa na kutokuwepo kwa ndugu wa familia yake kwani angelitaka wanaukoo wake wote wawepo katika msiba wake..
Mpwa wa marehemu Nelson Mandela, Mzwandile Mandela(13) ambaye anaishi jirani na nyumba aliyokuwa akiishi Mandela katika eneo la Qunu hakuruhusiwa kuhudhuria mazishi ya Mandela ikabidi atazame matukio yote kwenye Luninga kama anavyoonekana katika picha.
Hili ni eneo maalum ambalo watu wa ukoo na familia ya Marehemu Nelson Mandela huzikwa.
BAADHI YA WANAFAMILIA YA NELSON MANDELA WALALAMIKA KUTOALIKWA KATIKA MSIBA HUO KUTOKA NA HALI ZAO ZA MAISHA KUWA DUNI.
Reviewed by crispaseve
on
10:55 PM
Rating: 5
No comments:
Post a Comment