Header Ads

KINANA KUUNDA KAMATI KUSULUHISHA MGOGORO WA WANANCHI NA MGODI WA MAKAA YA MAWE MBINGA


 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana (wa tatu kushoto) na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk.Asha Rose Migiro (kulia) pamoja na wanaCCM wengine wakisaidia kulima shamba sehemu ya hekali 500 la Wajasiliamali vijana na wanawake wa Mbinga eneo laMkwaya,Kata ya Kilimani hao wamepewa shamba hilo na Jeshi la Magereza kwa ajili ya kilimo. Kinana na ujumbe wake wapo kwenye ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.

Wakulima wa shamba hilo wakisafisha shamba hilo tayari kwa kilimo eneo la Mkwaya, Kata ya Kilimani.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiangua kicheko baada ya kuchekeshwa na Mwanachama wa CCM Nafrolasa Luoga wakati Kinana na ujumbe wakae walipotembelea Shina la CCM la Balozi Hilda Komba, katika Kata Amani Makolo, wilayani Mbinga

Nape akisalimiana na baadhi ya wanachama wa shina hilo
 Wanachama wa Shina hilo wakila kiapo cha utii cha CCM baada ya kukabidhiwa kadi za kujiunga na chama hicho
Baadhi ya wananchni wa Kijiji cha Ntundualo wakigalagala cvhini baada ya kufurahishwa na Kinana ambaye aaliunda kamati ya kufuatilia tatizo la wananchi wa eneo hilo na Mgodi wa Makaa ya Mawe uliopo eneo la Rwanda, wilayani Mbinga ambapo wananchi hao wanadai fidia ya nyumba zao ili wapishe eneo hilo la mgodi.

Ngoma ya mganda ikitumbuiza wakati Kinana na ujumbe wake ulipowasili katika mgodi huo
 Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimatakifa, Dk. Asha Rose Migiro 9kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Intra Energy inayomiliki Mgodi  wa Makaa ya Mawe wa Ngaka, David Mason
Shughuli zikendelea katika mgodi wa makaa ya mawe
 Wasanii akina mama wa ngoma ya Chihoda, wakicheza mbele ya Kinana ikiwa ni ishara ya kumlaki alipowasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Mbinga.
 Akina mama wakicheza ngoma ya chihoda
Kinana akivishwa mgolole na Mzee Moris Mbunda ikiwa ni heshima ya kuwa mmoja wa wazee wa Mbinga
 Kinana akiwa na silaha za jadi alizopewa  kwa ajili ya kujilinda na kusafisha mafisadi
Kinana akijaribu moja kati ya pikipiki 50 alizokabidhi kwa vijana waendesha bodaboda . Pikipiki hizo za Mbinga Vijijini.ilizotolewa mkopo  zitasambazwa kwa kwa waendesha bodabod
 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Mbinga
 Dk Asha Rose Migiro akimkabidhi zawadi Balozi wa Shina la CCM la Amni Makoko, Hilda Komba
Mkazi wa Kijiji cha Ntundualo, ambaye ni mwanachama wa CCM, kadi namba 0753955521, Daniel Swemba akiwa ameshikilia kipeperushi  cha Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa alipokuwa akigombea urais mwaka 2000.Mzee huyo mwenye umri wa miaka 81 alisema kuwa ameamua kuwa na kipeperushi hicho baada ya kukosa kipya licha ya kujua kuwa Rais wa sasa ni Jakaya Kikwete.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA
 Kinana akihutubia wananchi wa Kijiji cha Ntundualo wilayani Mbinga. Kijiji hicho kipo ndani ya eneo la machimbo ya makaa ya mawe ya Ngaka eneo la Rwanda, wilayani Mbinga.
 Mbunge wa Mbinga Mashariki, Kayombo akihutubia katika mkutano huo na kumuomba Kinana kusaidia kuutafutiasuluhu mgogoro kati ya wanakiji wa Ntundualo na mgodi huo wa makaa ya mawe
Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Mbinga

No comments:

Powered by Blogger.