WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MH. KAGASHEKI AONGOZA MATEMBEZI YA SIKU YA TEMBO DUNIANI JIJINI ARUSHA YALIYO CHUKUA ZAIDI YA KILOMETA 4 LEO.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili
na Utalii Kahasheki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matembezi ya
amani ya Tembo Duniani kupinga mauaji ya Tembo hao.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili
na Utalii Kahasheki akionesha moja ya vibao ambavyo vinawaonesha Tembo
wakati wa Matembezi hayo ya amani.
Kutoka kushoto ni Mrs. Tibaijuka
akifuatiwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii
Kagasheki,Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Willbert
Chambulo, na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Muheshimiwa Magesa Mulongo.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa katika Matembezi ya Siku ya Tembo Duniani
Baadhi ya Wanaharakati wakiwa katika Matembezi ya siku ya Tembo Duniani
Ma elfu ya Wananchi kutoka Arusha
pamoja na wadau wengine kutoka Mikoa na nchi mbalimbali wakiwa katika
Matembezi ya siku ya Tembo Duniani yaliyo Fanyika Arusha Leo
Hawa ni Watoto Shupavu kabisa waliojitolea Mstari wa mbele katika Matembezi ya Tembo leo
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili
na Utalii Kahasheki akisaini katika moja la bango la siku ya Tembo ,
ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu
Maandamano yakiwa yanaendelea
Wa kwanza kutoka kushoto ni Mr.
Peter ambaye ndiye alikuwa katika kamati kuu ya Maandalizi ya Siku ya
Matembezi ya Tembo Duniani, na pia Makamu mwenyekiti wa Tanzania
Association of Tours operators akiwa katika matembezi hayo
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili
na Utalii Kahasheki akiongoza Ma elfu ya watu wakiingia katika viwanja
vya AICC ambapo ndipo ilikuwa kilele cha Matembezi hayo
Afisa Mtendaji wa Chama cha
Wakala wa Utalii TATO Ndugu Sirili Akko akitoa Maneno machache kabla ya
ufunguzi Rasmi wa Kilele cha Matembezi ya Tembo Duniani.
Meza kuu wakiongozwa na
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki wa nne kutoka
kushoto wakiwa wamesimama kwa mda wa dakika moja kuwakumbuka Waliokufa
katika Tukio la Westgate Kenya pamoja na Tembo walio uwawa .
Mc akiwa anaanza Tukio rasmi kwa kuwakaribisha viongozi mbalimbali kwa ajili ya Kutoa salam zao na Risala
Dr. Alfred kikoti Akitoa Mada
yake juu ya Idadi ya Tembo ambao wamebakia , pia kuelezea kutokomeza kwa
Biashara haramu ya uuzaji wa uuzaji wa Meno ya Tembo, na kusisitiza
Tanzania inategemea Tembo katika Utalii.
Mwenyekiti wa Tanzania Association
of Tours Operators Ndugu Wilbert Chambulo akielezea juu ya kusimamisha
biashara kubwa ya Meno ya tembo ambayo inaongozwa na Nchi ya China na
kuziomba Nchi zengine kusimamisha Biashara hiyo Haramu .
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Mongela wa Arusha Akimkaribisha Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Muheshimiwa
Magesa Mulongo akiwashukuru wananchi wa Arusha kwa kushiriki kikamilifu
zoezi la matembezi ya siku ya Tembo Duniani na kumkaribisha Mgeni Rasmi
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki kutoa hotuba yake.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na
Utalii Kahasheki akizungumza na wanaharakati waliofika katika siku ya
Matembezi ya Tembo Duniani, kwa kutoa Salamu kutoka kwa Muheshimiwa Rais
Kikwete kwamba Oparesheni ta kutokomeza majangili imeanza na
Haitasimama, alisisitiza kwamba Wanasheria wafunge midomo yao kuhusu
kutetea haki za binadamu , Aliongeza kwamba majangili wauwawe huko huko
wakikamatwa kurahisisha msongamano wa kesi mahakamani, na Mwisho
aliongeza kwamba Wanasiasa wasiingilie swala hili la kupambana na
ujangili.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akikabidhi vyeti kwa Shule Zilizo Shiriki Katika Matembezi ya Tembo Duniani
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na
Utalii Kahasheki akipokea zawadi kutoka kwa TATO Anaye mkabidhi zawadi
hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa TATO Mr. Peter
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mlongo akipokea zawadi kutoka TATO Anayemkabidhi ni Bi. Tibaijuka
Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za
Taifa Ndugu. Allan Kijazi akitoa neno la Shukurani wakati wa kufunga
Kilele cha siku ya Matembezi ya Tembo Duniani leo
Hawa ni Wale waliotembea katika
Matembezi ya Kupinga mauaji ya Tembo Kutoka Arusha hadi Dar es salaam
Mwendo wa Kilometa 650 kwa Siku 12 Kutoka kushoto ni Binti Mdogo mwenye
umri wa Miaka 20 Kaptorina Manange,Mkazeni Y. Mkazeni, Rehema Y. Najema,
na Livingstone Y. Mkazeni.
Maandamano haya yalitokea Jirani
na Cultural Heritage Hadi Viwanja vya AICC Kijenge Jijini Arusha,
Matembezi yaliyo andaliwa na Tanzania Association Tours Operators (TATO)
PICHA ZOTE NA BLOGS ZA MIKOA
No comments:
Post a Comment