VISION TANZANIA : PICHA ZA DR.SLAA ALIVYOTEMBELEA SHIRIKA LA UMEME NCHINI MAREKANI KATIKA JIMBO LA ALABAMA.
Dr. Slaa anaelekea kwenye ofisi za shirika.
Mkurugenzi mkuu akimpokea Dr. Slaa na Mkewe.
Pichani ni Mkurugenzi wa shirika akimpa maelezo Dr. Slaa jinsi shirika hilo linavyofanya kazi.
Sehemu maalum yenye ulinzi mkali ambako gridi inakuwa monitored.
Dr. Slaa akitizama kwa umakini
mitambo hiyo ya kusisimua inayoongoza gridi kusini mwa marekani.Hata
mashine moja ikiharibika watagundua maramoja na kuweza kutafuta njia
mbadala.
Dr. Slaa akikabidhiwa kitabu na mwanasheria mkuu wa shirika hilo.
Dr. Slaa anaendelea na safari yake
ya kujifunza inayoitwa “Vision Tanzania” ambayo leo imemfikisha katika
kituo kikubwa cha Umeme kinachoitwa Alabama Power Company ambayo
inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe,
upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia
Akielezea baadhi ya shuguli za Alabama Power company,
mkurugenzi wa shirika hilo linalojitegemea, ameeleza kwamba shirika hilo
linawahudumia wateja million nne tu, huku ikizalisha kiasi cha megawati
48,000 (4.8GW) Tangu kuanzishwa kwa shirika hilo, hakujawahi kutokea
mgao wa umeme au umeme kuzimwa hata kwa dakika 5. Panapotokea dharura,
kuna kuwepo njia mbadala ya kukabiliana nayo,
Kwa upande wake, Dr. Slaa amejifunza na kugundua kitu kimoja
kwamba, watanzania wanaumia kutokana na wachache kuligeuza Tanesco kuwa
mradi wao. Dr. Slaa anaamini kwamba mgao tulionao Tanzania, ukosefu wa
umeme tulionao ni matunda ya ufisadi wa CCM. Kiongozi huyo anaamini
kwamba tatizo ni ccm na desturi yao ya kulindana. ilahali tunatengeneza
600MW huku Waziri Muhongo akidai mwakani tutauza umeme nje ya nchi.
Umeme gani wa kuuza nje ya nchi wakati 80% ya watanzania hawana umeme?
Huyu mtu yuko katika sayari gani? Miaka 52 ya ufisadi, kugawana vyeo
kindugu, umasikini na magonjwa sasa tuseme basi. CCM hawawezi kujidai
kwamba watatatua matatizo ya watanzania
Viongozi wakuu Wizarani na Tanesco wanawazuia na
kuwadhalilisha wawekezaji kwa manufaa yao binafsi na makampuni
yasiyokuwa na huruma na mwananchi wa kawaida. Njia pekee ya kumuokoa
mtanzania, ni mtanzania mwenyewe kuamka, na kumng’oa adui CCM kupitia
njia ya kura. Mtanzania asifanye kosa tena 2015. Lazima amn’goe CCM ili
apate umeme na kuweza kuboresha maisha yake
Akitembelea mitambo inayopewa ulinzi wa kipekee, Dr. Slaa
amejionea jinsi kampuni hiyo inavyofanya shuguli zake pamoja na kuwa na
mitambo ya kisasa inayo monita njia zote za umeme kusini mwa marekani
yaani, Georgia, Florida, Alabama, Mississini na South Carolina.
Mkurugenzi wa shirika hilo, amemuahidi Dr. Slaa kwamba wako
tayari kuja Tanzania na kuisadia nchi hiyo kuboresha uzalishaji,
usambazaji pamoja na uendeshaji ikiwa serikali itawahitaji, kwani
wameisadia nchi za Philippines na Kuwait ambazo hadi sasa wanazo umeme
wa uhakika.
Picha na Habari kwa hisani ya Jamii Forums
No comments:
Post a Comment