Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa
Wateja itakayioanza Oktoba 7. Kushoto ni Meneja wa tawi la Premier,
Fabiola Mussula.
----
DAR ES SALAAM, Tanzania
Benki ya CRDB imezinduzi wiki maalum ya Huduma kwa Wateja ‘CRDB
Bank Customer Service Week’ itakayoanza kuanzia Oktoba 7 ambapo viongozi wa
benki hiyo watakuwa katika matawi na kusikiliza kero mbalimbali za wateja.
Wateja watakaofika mapema na kuhudumiwa katika matawi ya
benki ya CRDB watapata zawadi mbalimbali ambapo benki ya CRDB imeaandaa fomu
maalum kwa ajili ya wateja kutoa maoni yao kuhusu maeneo ambayo wangependa
yaboreshwe katika utoaji wa huduma.
Wateja watakaojaza fomu hizo na kutoa maoni au changamoto
nzuri watajishindia safari ya siku tatu kwenda visiwani Zanzibar ambayo
italipiwa na benki ya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dk.Charles Kimei amesema kuwa CRDB inaongozwa
na kauli mbiu yake “The Bank that Listens”.
“Katika kuendelea kuutambua mchango wa wateja watu, katika
wiki hii ambayo imepewa kauli mbiu ya “Je Umesikilizwa?, ambayo inalenga kuwapa
nafasi wateja kuongea kwa ukaribu na viongozi wa matawi na kutoa maoni yao
jinsi gani wangependa wahudumiwe” alisema Kimei na kuongeza kuwa katika wiki
hii viongozi wa juu wa benki watakuwa wakifanya kazi katika matawi yaliyopo
jijini Dar es Salaama katika mikoa mingine, pia fulsa hiyo itatumiwa na wateja
kufahamiana na viongozi wa juu wa benki hiyo.
Benki hio imekuwa kinara wa kuingiza sokoni bidhaa bunifu zenye
kukidhi mahitaji ya wateja kama vile mikopo mbalimbali inayolenga kuboresha
maisha na biashara zao.
Kusogeza huduma karibu zaidi na wateja kupitia njia
mbalimbali kama vile FahariHuduma (Agency Banking)Kuongeza njia za kutolea huduma, ikiweomo utumiaji wa njia
mbadala za kutolea huduma yaani “altenative Banking Channels” ikiwemo utoaji wa
huduma kupitia simu za mkononi yaani SimBanking, utoaji wa huduma kupitia
mtandao yaani Internet Banking, kupitia account Statement kwa njia ya mtandao
yaani E-Statement, kutoa huduma kwa kutumia matawi yanayotembea (Branch Wheels)
Kuendelea kuboresha mifumo ya utoleaji huduma, sasa hivi
mashine za kutolea huduma ni za uhakika zaidi na baadhi ya matawi yanatoa
huduma siku zote za wiki na hata siku za sikukuu kama vile tawi la Mlimani City
lililopo Dar es salaam, Vijana-Dar es Salaam, tawi la Mwanjelwa (Mbeya), Nyanza
(Mwanza) na Meru (Arusha).
Pia Benki ya CRDB imeboresha vituo vya huduma kama vile Call
Center ambayo hivi punde itaanza kufanya kazi kwa muda wa saa 24.
No comments:
Post a Comment