ZIARA YA MHE. HARRISON MWAKYEMBE NCHINI MAREKANI.
Mhe. Harrison Mwakyembe
alipotembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tanzania House,
Washington DC. Katikati ni Mhe. Waziri Harrison Mwakyembe akiwa na
ujumbe wake akiwa na baadhi ya maofisa wa Ubalozi huo Bw. Paul Mwafongo
(wa tatu Kushoto) na Bw.Suleiman Saleh (wa tatu kulia).
Mhe. Harrison Mwakyembe(Mb.)Waziri
wa Uchukuzi akipokewa na mwenyeji wake Bw.Robert Shumake,Balozi wa
Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Michigan mara baada ya
kuwasili hotelini alikofikia.
Mhe.Waziri Mwakyembe katika picha ya pamoja na Bw. Shumake na Bw. Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ,Washington DC.
Juu na chini ni Mhe. Mwakyembe
katika taswira mbali mbali na Bw. Joelson, Mmiliki wa kituo cha
kufundisha Urubani cha DCT katika ziara yake kituoni hapo ambapo
alionyeshwa ndege za aina mbali mbali pamoja na kupata historia ya kituo
hicho.
Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati)
na Ujumbe wake Bw. Peter Lupatu , Mkurugenzi wa Huduma za
Usafiri,Wizara ya Uchukuzi, Bw.Suleiman Saleh Afisa wa Ubalozi wa
Tanzania Washington DC, Eng.K . Kisamfu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Reli la Tanzania, Bw. Mohamed Millanga, Mkurugenzi wa Mradi (Terminal
3 Building), na Bw. Andrew Magombana katika picha ya pamoja na viongozi
wa Kampuni ya General Electric ya Erie, Pennsylvania.
Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Mheshimiwa Dk.Harrison
Mwakyembe(Mb.),Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
amefanya ziara ya kikazi nchini Marekani katika miji ya Washington DC,
Erie, Pennsylvania na Detroit, Michigan, kuanzia tarehe 18 -22
Septemba, 2013, kwa mwaliko wa Bw. Robert Shumake, Balozi wa Heshima wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jimbo la Michigan. Wakati wa
ziara hiyo, Mhe.Mwakyembe ambaye alifuatana na Bw. Lupatu, Mkurugenzi wa
Huduma za Usafirishaji katika Wizara ya Uchukuzi, Eng. K. Kisamfu,
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli la Tanzania, Bw. Mohamed
Millanga,Mkurugenzi wa Mradi, Terminal Building 3, na Bw. Andrew
Magombana,
Msaidizi wa Waziri . Mhe.Mwakyembe
alipata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
uliopo Washington DC na kisha kusafiri hadi Erie,Pennsylvania, kufanya
mazungumzo na uongozi wa Juu wa kampuni ya General Electric
inayotengeneza injini za treni. Katika mkutano wake huo Mhe.Mwakyembe
na ujumbe wake ulipata fursa ya kuelezwa shughuli mbali mbali za kampuni
hiyo pamoja na kutembelea karakana kuu ya kampuni hiyo yenye watumishi
zaidi ya laki tatu. Akiwa mjini Erie, Mhe.Mwakyembe alipata fursa ya
kueleza mikakati iliyopo ya kuliboresha Shirika la Reli la Tanzania
pamoja na kujenga mashirikiano zaidi baina ya kampuni na Serikali ya
Tanzania katika kukamilisha azma hiyo. Baadae Mhe. Mwakyembe na ujumbe
wake ulisafiri hadi katika mji wa Detroit,Michigan, ambapo alipokelewa
na alifanya mazungumzo na Bw.Shumake,Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mwenye makazi yake katika mji wa Detroit. Akiwa
mjini humo Mhe. Mwakyembe alitembelea kituo cha mafunzo ya Urubani
ambapo alielezwa historia ya kituo hicho pamoja namna ambayo kituo hicho
kitasadia katika kuanzisha kituo cha Mafunzo ya Urubani nchini
Tanzania. Aidha Mhe.Mwakyembe alipata wasaa wa kuonyeshwa aina ya ndege
mbali zinazotumika katika mafunzo hayo. Kituo hicho kimetoa mafunzo
mafunzo kwa marubani 3500 tangu kianzishwe miaka kumi na nane iliyopita.
No comments:
Post a Comment