WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo
Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika
Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kumpa pole, baada ya
kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa
wa Mjini Magharibi, Zanzibar wiki iliyopita. Dk Nchimbi alimtoa hofu
Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na
serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote
kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya
tindikali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimsikiliza Padri Joseph Monesmo
Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, akitoa maelezo
jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa Tindikali na watu wasiojulikana, Mjini
Unguja, Zanzibar alipofika katika Hospitali ya Muhimbili kumpa pole,
ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu. Dk Nchimbi alimtoa hofu Padri
huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo watakamatwa, na
serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi chochote
kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali ya
tindikali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimuhakikishia Padri Joseph Monesmo
Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Zanzibar jinsi
wizara yake itakavyopambana kwa kuwakamata wale wote watakaojihusisha na
vitendo vya uhalifu wa kutimia kemikali ya tindikali. Dk Nchimbi
alifika hospitalini. Dk Nchimbi alifika katika Hospitali ya Muhimbili
jijini Dar es Salaam kumpa pole padri huyo ambaye anatarajiwa kupelekwa
nchini India kwa ajili ya kupata matibabu zaidi. Hata hivyo, Dk Nchimbi
alimtoa hofu Padri huyo akimuahakikishia kuwa waliofanya tukio hilo
watakamatwa, na serikali itapambana kikamilifu na mtu au kikundi
chochote kitakachojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia kemikali
ya tindikaliPicha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment