ASKARI WA JWTZ ALIYEJERUHIWA CONGO NA KUFARIKI AAGWA LUGALO
Askari
Jeshi
la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili
wa Askari mwenzao, Marehemu Private, Hugo Munga alifariki dunia Septemba
18
mwaka huu huko Pretoria Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata
akiwa na
vikosi vya MONUSCO Congo DRC katika operations ya kuwaondoa waasi wa
M23. Mwili
wa Munga ulisafirishwa jana kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu ilifanyika Viwanja vya Jeshi
Lugalo, Dar es Salaam.
Mama wa Marehemu, Jovitha Barnaba Munga akisaidiwa kuaga mwili wa mwanae.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange akizungumza
Baadhi ya waombolezaji ambao ni
Askari wenzake marehemu pamoja na wana familia wakiwa eneo la
tukio.Picha Kwa hisani ya Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment