President Kikwete meets MCC CEO and Oman's Foreign Minister in New York
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets the CEO of the Millenium Challenge Corporation (MCC) Mr.Daniel Yohannes in New York |
Zanzibar's
Minister for Labour, Economic Empowerment and Cooperation Mr.Haroun Ali
Suleiman meets MCC CEO Mr.Daniel Yohannes in New York
President
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets and hold talks with the Foreign Minister
of the Sultanate of Oman Mr.Yousef Bin Alawi Bin Abdullah in New York
Rais
Kikwete: Tunaifanyia mageuzi makubwa TANESCO
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa
Serikali yake inalifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) kwa nia ya kuharakisha jitihada za Serikali kusambaza
umeme kwa wananchi wengi zaidi.
Aidha, Rais
Kikwete amesema kuwa Serikali imechukua hatua nyingi na kali za kupambana na
rushwa kwa nia ya kukomesha vitendo hivyo katika Tanzania na kuinua kiwango cha
utawala bora.
Rais Kikwete
ameyasema hayo Jumatano, Septemba 25, 2013 wakati alipokutana na
kuzungumza na ujumbe wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani la Millennium Challenge Corporation (MCC)
ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Bwana Daniel W Yohannes.
Ujumbe huo
umekutana na Rais Kikwete katika Hoteli ya JW Marriott mjini New York ambako
Rais Kikwete amefikia kwa ziara yake ya kikazi katika Marekani ambako miongoni
mwa mambo mengine atahutubia Mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) ulioanza jana, Jumanne, Septemba
24, 2013.
Katika
mazungumzo hayo, Bwana Yohannes amemwelezea Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya
ombi la Tanzania kuingizwa katika awamu ya pili ya misaada ya Serikali ya
Marekani kupitia MCC chini ya Akaunti
ya Milenia Tanzania (MCA(T)). Nchi
nyingine za Afrika ambazo maombi yao yanafikiriwa katika awamu hiyo ya pili ni
Morocco, Mozambique na Lesotho.
Tanzania ndiyo
nchi iliyopokea sehemu kubwa zaidi ya msaada wa MCC duniani katika awamu ya kwanza ambako ilipewa kiasi cha dola za
Marekani milioni 698 ambazo zimeingizwa katika miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara,
usambazaji wa umeme vijijini, miradi ya maji na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa
Mafia.
Serikali ya
Tanzania imeamua kuwa fedha za awamu ya pili ya MCC zitaingizwa kupanua zaidi huduma za umeme na ujenzi wa barabara
za vijiji kwa nia ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaopata huduma za umeme na
kwa nia ya kuboresha barabara za vijijini katika maeneo yanayozalisha mazao kwa
wingi zaidi.
Serikali ya
Rais Kikwete imeliweka suala la usambazaji umeme kwa Watanzania mijini na
vijijini miongoni mwa maeneo yake ya kipaumbele. Wakati anaingia madarakani
mwaka 2005, ni asilimia 10 tu ya Watanzania waliokuwa wanapata umeme. Katika
miaka saba iliyopita, asilimia hiyo imepata hadi kufikia 21 ikiwa ni asilimia
11 zaidi kuliko katika miaka yote 50 ya Uhuru. Lengo la sasa ni kuifikisha
asilimia 30 ama zaidi mwaka 2015.
Katika
mazungumzo hayo na Rais Kikwete, Bwana Yohannes ametaka kujua ni hatua zipi
Serikali inazichukua kurekebisha changamoto zinazoikabili TANESCO na hatua gazi
zinachukuliwa kuzidi kukabiliana na matatizo ya rushwa.
Rais Kikwete
amemweleza Bwana Yohannes: “Kama unavyojua, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
limepitia safari ngumu na kukabiliwa na changamoto nyingi lakini sasa tumeamua
katika Serikali kulifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa kwa maana ya
muundo wake na pia kuangalia viwango vya malipo ambayo Shirika hilo linawatoza
wateja wake. Mageuzi haya katika TANESCO ni muhimu sana na yameanza kufanyika
na kwa hakika Serikali imedhamiria kukayamilisha mageuzi hayo katika muda mfupi
iwezekanavyo.”
Kuhusu rushwa,
Rais Kikwete amemwambia Bwana Yohannes, “Jitihada zetu katika kupambana na rushwa
zinaendelea. Tumeimarisha taasisi inayohusika na kuzuia na kupambana na
rushwa.Tumeimarisha mtandao wa kukabiliana na balaa hili na Serikali yangu
imewafikisha mahakamani waliopata kuwa viongozi na maofisa waandimizi wa umma
katika Serikali kujibu mashitaka ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment