MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA AFUNGUA KAMBI YA VIJANA WA CCM HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akishiriki kwa vitendo
kufyatua matofali na vijana wa CCM walioweka kambi katika Halmashauri ya
Wilaya ya Sumbawanga katika Mji mdogo wa laela tarehe 22 Septemba
2013. Lengo kuu la kambi hiyo ni kuwajenga vijana katika itikadi na sera
za Chama cha Mapinduzi, Ukakamau na Uzalendo kwa chama na nchi yao kwa
ujumla. Katika kambi hiyo wanajishughulisha pia na kazi za kijamii kama
kufyatua matofali zaidi ya 6,000 yatakayosaidia katika kujenga kituo cha
afya Laela. Katika kuwapa nguvu kuendeleza kambi hiyo Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa alitoa mchango wa laki mbili taslim.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Mbunge viti maalum CCM Mkoa wa Ruvuma
akiwahamsisha vijana hao kukipenda chama chao kwa kuweka uzalendo mbele
katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Chama hicho katika mji mdogo
wa Laela tarehe 22 Septemba 2013. Kutoka kushoto ni Matin Matete Mjumbe
wa baraza kuu CCM taifa, C. Bakuli Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Rukwa,
Injinia Manyanya RC Rukwa, Godwin Mzurikwao Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa
Rukwa, Ali Mgaya Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
Vijijini na Persin Kalikule Mhamasishaji UVCCM Mkoa wa Rukwa.
Sehemu
ya vijana hao waliotoka katika maeneo tofauti ya Halmashauri ya Wilaya
ya Sumbawanga wakionekana kuhamasika vya kutosha katika kambi hiyo
iliyopo katika mji mdgo wa Laela.
Mwenyekiti
wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa (UVCCM) Godwin Mzurikwao
akielezea mipango mbalimbali ya umoja huo ikiwemo uhamasishaji na
upandaji miti ya mbao kwa ajili ya kuwainua vijana kiuchumi Mkoani
Rukwa. Katikati akisikiliza kwa umakini ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi ndugu Ali Mgaya
Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini miti na
viriba vya kupandia miti ya mbao ambayo ni sehemu ya mpango wa UVCCM
Mkoa wa Rukwa kuwawezesha na kuwahamasisha vijana katika zoezi la
upandaji miti wa kibiashara.(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa....rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment