CHIKAWE AMKIMBIA MAKAMU WA RAIS, MCHEZO WA KAMBA WANANWAKE SHIMIWI DOM, WANAUME OMR WAWABURUZA KATIBA NA SHERIA
Baadhi ya wachezaji wa timu ya
Kamba ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakishangilia ushindi wao baada ya
kuwaburuza timu ya Katiba na Sheria katika raundi mbili mfululizo,
katika mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu
cha UDOM mjini Dodoma.
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya
Makamu wa Rais, Kamba wakionyesha uwezo wao wa kutunisha misuri
kuwaburuza wapinzani wao wa timu ya Katiba na Sheria, wakati wa mchezo
wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini
Dodoma. Katika mchezo huo Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda kwa raundi
mbili mfululizo.
Wachezaji wa timu ya Katiba na
Sheria, Kamba wakijaribu kugangamala kuwazuia wapinzani wao wa timu ya
Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa mchezo wao uliochezwa leo asubuhi
kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Katika mchezo huo
Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda kwa raundi mbili mfululizo.
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya
Makamu wa Rais (kulia), Kamba wakionyeshana umwamba wapinzani wao wa
timu ya Katiba na Sheria, wakati wa mchezo wao uliochezwa leo asubuhi
kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Katika mchezo huo
Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda kwa raundi mbili mfululizo.
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya
Makamu wa Rais Kamba wanawake, wakishangilia ushindi wa chee waliopata
baada ya wapinzani wao Katiba na Sheria kuingia mitini.
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya
Makamu wa Rais, Kamba na Soka, wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya
timu zao za Kamba (KE) na (ME) kushinda katika michezo yao.
Kamba wananwake Bunge na
Uchukuzi, wakiburuzana. Katika mechi hii, Bunge walishinda baada ya
kuwaburuza wenzao mara mbili mfululizo.
'RAHA YA USHINDI BAO', Wachezaji
wa timu ya Kamba ya Habari, wanaume wakishangilia ushindi wao baada ya
kuwaburuza mara mbili mfululizo wapinzani wao, Uhamiaji katika mchezo
wao uliochezwa leo asubuhi, kwenye viwanja vya Chuo Kikuu UDOM, mjini
Dodoma.
Wachezaji wa timu ya Habari
(kushoto), Kamba wakionyeshana umwamba wapinzani wao wa timu ya
Uhamiaji, wakati wa mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya
Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Katika mchezo huo Habari ilishinda
kwa raundi mbili mfululizo.
Mchezaji wa timu ya wanawake
Kamba ya Uhamiaji, akibebwa kuwekwa pembeni ili kupatiwa huduma ya
kwanza baada ya kuanguka wakati walipoburuzwa na wenzao wa Habari na
kuwavuta mara mbili mfululizo, katika mchezo wao uliochezwa kwenye
Viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM leo asubuhi.
Uhamiaji wanawake wakijaribu kugangamala kuwazuia Habari, lakini waliburuzwa katia mechi hiyo.Picha Zote na OMR
*****************************************
Na www.sufianimafoto.com
TIMU ya Kamba ya Ofisi ya Makamu
wa Rais, Wanawake leo imeibuka na ushindi wa mezani baada ya timu ya
kamba wanawake ya Katiba na Sheria kuingia mitini.
Mwamuzi wa mchezo huo alipuliza
kipyenga na kutoa ushindi huo kwa timu hiyo ya Ofisi ya Makamu wa Rais,
wanawake baada ya kuita timu zote kuingia uwanjani kwa ajili ya
kucheza na kujitokeza timu moja ambayo ilipewa ushindi wa bure. Kwa
ushindi huo sasa timu hiyo ya Wanawake OMR, inatarajia kucheza na timu ya Bunge kesho katika viwanja vya Chuo Kikuu UDOM.
Wakati wanawake wa Ofisi ya Makamu
wa Rais wakipata ushindi wa chee, wenzao wanaume pia wameshinda mchezo
huo kwa kuwaburuza bila huruma timu ya Katiba na Sheria wanaume, katika raundi zote mbili mfululizo.
Timu ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa
Rais inashuka dimbani leo mchana saa nane kutupa karata yake ya kwanza
kwa kukipiga na Mambo ya nje, mchezo utakaochezwa kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma.
Akizungumza na mtandao huu, Kocha
wa timu hiyo, Ucheche, alisema kuwa amekiandaa kikosi chake chenye
wachezaji wazoefu waliojipanga kuonyesha soka la ukweli jioni ya leo.
Aidha aliwataja baadhi ya
wachezaji wanaokiwakilisha kikosi chake kuwa ni pamoja na Jumanne,
Mhina, Kihoko, Issa, Sufiani, Lucas, Kifaru, Mandia, Kibik, Mascat na wengineo.
No comments:
Post a Comment