CHF YAKUBALIKA KAMA SULUHISHO LA MATIBABU NYEGENDI MKOANI LINDI
Wananchi
wa Kata ya Nyengedi Lindi wakimsikiliza Mh. Nawanda DC wa Lindi
akiwaelimisha umuhimu wa CHF katika kampeni ya uhamasishaji unaofanywa
na NHIF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo
Mkuu
wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya Nawanda akiwasikiliza akisikiliza kwa
makini hoja za wana Nyengedi ili kupata mrejesho wa huduma za afya
katika kata hiyo. wakati alipokuwa akiwaelimisha kuhusu umuhimu wa
huduma za CHF katika kampeni ya uhamasishaji inayofanywa na NHIF kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo
Mkuu
wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya Nawanda akisisiztiza jambo wakati NHIF
ilipozindua kampeni hizo katika wilaya ya Lindi mkoa wa Lindi kulia ni
Mkuu wa mkoa huo Mh. Jordan Lugimbana na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa na Eugine Mikongoti Mkurugenzi wa wa
Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii
Tanzania, NHIF
Wana Nyengedi wakipima ili kujua afya zao katika kampeni ya CHF.
Wanakijiji
wa Nyengedi wakidunduliza fedha ili kufikisha mchango wa sh. 10,000 kwa
kaya ili wajisajili na CHF baada ya kuhamasika.
............................................
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kishirikiana na Halmashauri ya Lindi
Vijijini wameendelea na kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na
Mfuko wa Afya ya Jamii CHF katika kata ya Nyangedi.Katika uhamasishaji
huo uliongizwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Nawanda kaya 70 zilijiunga
papo hapo kwa kuchangia Shilingi 10,000 kwa kaya hivyo jumla ya Shilingi
700,000 zilikusanywa.
Aidha
Mh. Nawanda alimwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha hakuna
upungufu wa dawa katika kituo hicho na endapo litatokea hilo wananchi
wamjulishe mapema.
Pia aliwakumbusha maagizo ya Mkuu wa Mkoa kwamba wasiojiunga na CHF
watalipia Sh. 10,000 kwa matibabu kila wanapoenda kutibiwa kama hawaoni
umuhimu wa kuchangia 10,000 kwa kaya kwa mwaka mzima na wakatibiwa kwa
kadi.
Alimaliza kwa kuwahimiza watu kufanya kazi kwa bidii ili waweze kutimiza mahitaji yao kama afya kwani fursa za uzalishaji zipo.
Uhamasishaji wa CHF unaendelea katika kata mbalimbali za Lindi katika
wiki hìi na baada ya hapo katika Halmashauri mbalimbali nchini.




No comments:
Post a Comment