RC Makalla atembelea kiwanda cha sukari TPC, akerwa na sukari inayoingia kwa wingi kutoka nje
MKUU wa Mkoa
Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara katika kiwanda cha Sukari cha TPC kilichopo
Moshi, mkoani Kilimanjaro ili kujionea hali ya uzalishaji wa sukari kwenye
kiwanda hicho. RC Makalla
alijionea hali halisi ya kiwanda hicho ambacho sasa kinazalisha sukari tani
105,000 baada ya kubinafsishwa, tofauti na uzalishaji wa tani 35,000 tu hapo
zamani.
Ziara inaendelea kiwandani hapo.
Akizungumza
katika kiwanda hicho, RC Makalla alisema kwamba amefurahishwa na hali
ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho, huku akiahidi kushirikiana
na uongozi wa Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari inayoingia kutoka nje ya
nchi. Alisema atashirikiana na
serikali ya Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari hiyo ya nje, akiamini kuwa
kutasababisha kiwanda hicho kupiga hatua kwa kuuza sukari yao nchini.
Majadiliano yanaendelea kiwandani hapo dhidi ya RC Makalla
“Kilio
cha kiwanda hiki ni uingizwaji wa sukari kutoka nje, hivyo Kilimanjaro
tutashirikiana kwa karibu na wenzetu wa Tanga ili kuweka ulinzi mkali
kwa ajili ya kudhibiti sukari inayoingia kutoka nje kwa kupitia mkoani
Tanga.



No comments:
Post a Comment