Header Ads

Timu ya Zanzibar Diaspora USA Yanyakua Kombe la Muungano Washington DC, Kwa Ushindi wa Mabao 7-1 dhidhi ya Tanganyika

Katika shamrashamra za kusherehekea Miaka 51 kuungana Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Timu ya Zanzibar Diaspora​ nchini Marekani imeifunga bao 7-1 jirani zake timu ya Tanganyika USA.
Kocha wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir pamoja na Kapteni Deddy Rouba​ wakikabidhiwa Kombe la Muungano.

Mechi hiyo ambayo imehudhuriwa na mgeni rasmi rais mstafu wa awamu ya pili wa Tanzania Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi. ilifanyika katika viwanya vilivyopo Walker Mill Road District Heights Maryland, ambapo pia ilihudhuriwa na balozi wa Tanzania nchini Marekan Mhe. Liberata Mulamula.

Mechi hizo hufanyika kila mwaka kwaajili ya kusherehekea kuungana kati ya Tanganyika na Zanzibar April 26, 1964.
Rais mstafu wa awamu ya pili wa Tanzania Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi baada ya kusalimiana na wachezaji wa timu zote mbili

Mapema Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi aliwataka waTanzania kuungana kwa pamoja bila ya kujali tafauti zao.Wakati huo huo kabla ya mechi kuaza Alhajji Ali Hassan Mwinyi alisalimiana na timu zote mbili na kuupiga mpira kuashiria kuaza kwa mechi hiyo.
Kikosi kamili cha timu ya Zanzibar Diaspora
Mashindao hayo ambayo yaliwapa ushindi mnono Timu ya Zanzibar Heroes baada ya kichapo cha 7-1 dhidi ya Timu ya Tanganyika katika mechi ya kutafuta Bingwa wa Kombe la Muungano, bao la kwanza kwa timu ya Zanzibar lilifungwa kwa njia ya Penalti mfungaji wa bao hilo alikuwa Yahya Kheri na magoli mawili ya lifungwa na Wingi machachari Abdulla J. Somania, mbao hadi timu kipindi cha kwanza kumalizika Timu ya Tanganyika ilifungwa 3-0

No comments:

Powered by Blogger.